Wachezaji wa Uholanzi wakipozi katika picha huku wakiwa na medali zao baada ya kuitandika Brazil mabao 3-0 na kushika nafasi ya tatu katika fainali za kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil.
Mshindi: Kocha wa Uholanzi Louis van Gaal akipokea medali kutoka kwa rais wa FIFA, Sepp Blatter.
Ndoto zilianzia hapa: Nahodha wa Uholanzi, Robin van Persie alifunga bao la kuongoza kwa mkwaju wa penati na kumuacha kipa Julio Cesar akiambulia unyoya tu. Chezea RVP weyeeeeeeeeeeeee!
Maboya: Kipa wa Brazil, Julio Cesar akishindwa kuokoa penati ya Robin van Persie katika dakika ya 3 ya kipindi cha kwanza.
Oyooo! wamekalishwa tena! : Robin van Persie akishangilia bao lake na mchezaji mwenzake Dirk Kuyt (aliyempanda juu)
Hesabau tu!: Beki wa Uholanzi, Daley Blind akipiga shuti kuandika bao la pili dhidi ya Brazil.
Freshi sana wana!: Daley Blind (wa pili kushoto) akishangilia baada ya kuifungia Uholanzi bao la pili dhidi ya Brazil
Beki wa Uholanzi alipata majeraha wakati akichuana na Oscar wa Brazil (kushoto).
Kingine hicho: Kiungo wa Uholanzi, Georginio Wijnaldum akifunga bao la tatu na la ushindi katika dakika za majeruhi.
Kaah! si majanga haya jamani, umefanya nini Georginio Wijnaldum?
Toa Maoni Yako:
0 comments: