Mchezaji Lionel Messi ambaye aliitoa kimasomaso timu yake, akishangilia ushindi.

Argentina wakishangilia baada ya kutinga fainali kwa ushindi wa penalti 4-2.
Messi kazini: Lionel Messi akijaribu kumtoka Nigel de Jong wakati wa mtanange huo.
Kiwango: Nahodha wa Uholanzi Robin van Persie akimiliki mpira dhidi wa wachezaji wa Argentina.
Hakatizi mtu: Mshambuliaji wa Uholanzi, Arjen Robben akifanyiwa madhambi na beki wa Argentina, Martin Demichelis.

Hero to zero: Vlaar's impressive display was overshadowed by his failure from 12 yards
Nightmare start: Vlaar looks on as Sergio Romero guesses the right way to keep out his kick
Kipa akitoa pande...
Hero: Romero denied Vlaar and Wesley Sneijder in the shootout
Pozi: Mashabiki wa Argentina wakipozi kabla ya mtanange huo.
TIMU ya Argentina imetinga fainali ya michuano ya Kombe la Dunia 2014 baada ya kuiondoa Uholanzi kwa penalti 4-2 kwenye mchezo wa nusu fainali uliopigwa Sao Paulo, Brazil usiku huu.
Kipa wa Argentina, Sergio Romero, alifanikiwa kuokoa mikwaju miwili ya penalti iliyopigwa na Ron Vlaar na Wesley Sneijder wa Uholanzi baada ya dakika 120 kumalizika timu hizo zikiwa suluhu.
Lionel Messi, Ezequiel Garay, Sergio Aguero na Maxi Rodriguez waliifungia Argentina kwa penalti huku Waholanzi Arjen Robben, Dirk Kuyt wakifunga penalti za Uholanzi.
Kwa matokeo ya leo, Argentina watamenyana na Ujerumani katika fainali itakayopigwa Julai 13 mwaka huu huku Uholanzi na Brazil wakipepetana kuwania nafasi ya mshindi wa tatu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: