Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia akinyanyua juu cha kitabu cha "HISTORIA YA SIMBA" kuashiria uzinduzi wa kitabu hicho. Uzinduzi huo uliofanyika leo Julai 16, 2014 katika Club ya Simba jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia kulia ni mtunzi wa kitabu hicho Mwina Kaduguda, Mkurugenzi wa Mkuki na Nyota Bw. Mkuki Bgoya ambao ndio wachapishaji wa kitabu hicho pamoja na Mjumbe wa TFF.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Klabu ya Simba, Bw. Collin Frisch akiongea kwa niaba ya Rais wa Simba, ambapo amempongeza mtunzi wa kitabu Mwina Kaduguda kwa kuweiweka Klabu ya Simba kwenye Kumbukumbu muhimu ya maandishi. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Mkuki na Nyota, Bw. Mkuki Bgoya, Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Juma Nkamia na Mjumbe wa TFF.
Mkurugenzi wa Mkuki na Nyota Bwana Mkuki Bgoya akieleza machache mbele ya waandishi wa habari wakati wakizinduzua kitabu hicho.
Mtunzi wa kitabu cha "HISTORIA YA SIMBA", Bw. Mwina Kaduguda akielezea changamoto alizozipata kwa muda wa miaka saba wakati akiandaa anaandaa kitabu hicho. Ambapo alisema dhumuni kubwa la Kutunga kitabu hicho ni kutunza historia ya soka ya Timu hiyo isipotee ili iweze kusomwa kizazi na kizazi. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Juma Nkamia, Mkurugenzi wa Mkuki na Nyota Bw. Mkuki Bgoya ambao ndio wachapishaji wa kitabu hicho.
Mtunzi wa Kitabu cha "HISTORIA YA SIMBA", Bw. Mwina Kaduguda akimkabidhi Kitabu chake Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia Zawadi ili ampekelekee Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia akitoa neno kumpongeza Mwina Kaduguda kwa kufikiria mbali sana kwa kuweka soka la Tanzania kwenye maandishi namna klabu ya simba ilivyoanza, Pia aliongeza kuwa Klabu za soka Tanzania zinatakiwa kuwa na watu kama Mwina Kaduguda ili kuleta maendeleo ya soka na kila mwanachama kujituma kwa bidii na kuacha kukaaa kwenye korido za Klabu na kupiga Zoga.
Mwandishi wa Habari wa Shirika la Habari la BCC, Arnold Kayanda akifanya mahojiano na Kamati ya Utendaji Klabu ya Simba, Bw. Collin Frisch jinsi walivyokipokea kitabu hicho. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
---
Historia ya Klabu ya Simba Tangu 1920 hadi 2014
Mwandishi: Mwina Kaduguda
Mchapishaji: Mkuki na Nyota Publishers
Mwaka: 2014
Kurasa: 128
Bei: Shilingi 15,000/=


Muhtasari wa Kitabu

Hiki ni kitabu cha kwanza chenye historia ya kina ya Simba Sports Club. Kama mpenzi wa soka, hususan mkereketwa wa Simba, utajua chimbuko na undani wake tangu ilipoanzishwa hadi hii leo. Vilevile utaweza kutumia kitabu hiki kama ushahidi katika mabishano na mijadala inayohusiana na klabu, wachezaji, viongozi, timu pinzani na bila kusahau historia ya soka la Tanzania kwa ujumla.


Utasoma vioja vya soka letu kama vile ushabiki wa kupindukia, vituko na imani za kishirikina, makundi yaliyotia fora, migogoro, mafanikio, picha za matukio mbalimbali, bila kusahau rekodi za mwenendo wa timu na misimamo ya ligi katika historia ya klabu.



Kwa kukisoma kitabu hiki utafahamu pia mambo mengi yanayolizunguka soka la Tanzania, kwani rekodi hizi hazipatikani kwa urahisi na mwandishi ametumia muda mwingi kufanya utafiti na kukusanya taarifa kutoka vyanzo mbalimbali rasmi kama vile maktaba, vitabu, magazeti, nyaraka na kuwahoji wazee wa zamani. Kwa mfano, utajua ni lini soka liliingia na kusambaa nchini katika karne ya 20, mpasuko uliozaa Simba na Yanga na mengine mengi ya kuburudisha, kuelimisha na kusisimua.



Kuhusu Mwandishi

Mwina Mohamed Seif Kaduguda, mzaliwa wa Kasulu, Mkoa, wa Kigoma ana shahada ya Bachelor of Arts (B.A. Hons), Ushirikiano wa Kimataifa na Utawala, UDSM 1992, Cheti cha Uandishi wa Habari-TSJ, 1994. Ana Diploma ya Ukocha wa Soka HUPE-Budapest, Hungary 1997, Cheti cha Utawala wa michezo-IOC, 2001, Cheti Cha Uamuzi wa Soka-FRAT, 2001 na Cheti Cha Juu cha Ukocha-CAF, 2006.


Ameshika nafasi nyingi za uongozi wa Mpira wa Miguu nchini zikiwamo zile za Katibu Mkuu FAT sasa TFF, 2003–2004, Katibu Mkuu TAFCA, 2002–2008, Katibu Mtendaji SPUTANZA, 2001–2004, Katibu Mkuu TASWA, 1997–2004 Mkufunzi Msaidizi wa Makocha wa soka TFF, 2006, Katibu Mkuu SIMBA S.C., 2006–2010 na Mjumbe BMT, 2000–2005. Ameshiriki katika makongamano ya kimataifa ya michezo Toronto-Canada, Athens-Ugiriki, Kuala Lumpur-Malaysia na Sandton City-Afrika ya Kusini.



Hivi sasa ni mwalimu katika Shule ya Sekondari ya Jitegemee, Dar es Salaam na anapatikana kwa mahojiano na majadiliano kuhusu mada mbalimbali zilizomo kitabuni.


KWA TAARIFA ZAIDI AU MANUNUZI YA JUMLA NA REJA REJA WASILIANA NA:
Mkuki na Nyota Publishers Ltd
Simu: 0787558448
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: