Siku chache baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kuifutia leseni Kampuni ya Uwindaji wa kitalii ya Green Mile Safari limited kwa tuhuma za uwindaji usiozingatia sheria za wanyamapori, Uongozi wa kampuni hiyo umesema unatarajia kwenda mahakamani kudai haki ya kurudishiwa leseni hiyo kama ngazi ya juu ya serikali haitaweza kulishughulikia suala hilo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Mwanasheria Alloyce Komba ameeleza kwamba tuhuma walizo pewa wao kupitia DVD iliyotolewa na Waziri kivuli wa Utalii Peter Msingwa hazikustahili kwani shughuli nzima za uwindaji wa kitalii zinasimamiwa na mtaalamu wa uwindaji pamoja na askari wa wanyamapori.

Aidha mwanasheria huyo amesema kuwa wao kama wa husika wakuu wameshangaa kuona Kwa uamuzi wa Waziri Nyalandu wa kuwafutia leseni bila ya wao kutoa maelezo au kisikilizwa juu ya tuhuma hizo.

Kampuni hiyo imeeleza kwamba wao wanaamini chimbuko la sakata hilo la kufutiwa leseni limekuja kutokana na mgogoro wa kitalu cha Lake Natron Game Controlled Area ambacho kampuni ya kigeni wengert Windrose Safari limited ilikuwa ima miliki hapo awali.

Hivi karibuni Waziri kivuli wa Utalii Mchungaji Msigwa alitoa DVD iliyoonyesha uwindaji uliofanyika kinyume na sheria.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: