Hoteli ya Naura Spring - Arusha Haujaungua kwa moto kama watu ambavyo wamezusha kwenye mitandao ya Jamii.

Baada ya Kajunason Blog kuona habari zimesambaa katika mitandao ya kijamii, tuliweza kuwasilia na mmoja ya viongozi wa hoteli hiyo ambaye hakupenda kutaja jina lake, alisema amesikitishwa sana jinsi watu walivyosambaza habari hizo za uongo kuichafua hoteli yao.

"Kiukweli nimesikitishwa na jinsi ambavyo watu wanasambaza maneno ya uongo uongo na watu wametengeneza picha za uongo kuonyesha hoteli inaungua jambo ambalo si la kweli," Alisema mtoa habari.

Kajunason inapenda kutoa ushauri kwa Blogger's na Watanzania kwa ujumla kuacha kukurupuka pindi wanapoona jambo kwenye mitandao ya jamii.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: