Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania Kanda ya Mashariki, Julius Nyaga kushoto akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Schalke 04 ya Dodoma, Mussa Gaidi baada ya timu yake kushika nafasi ya kwanza ya Castle Lager Perfect Six kutoka kanda ya Kati katika michezo iliyofanyika uwanja wa Fire Morogoro kwa kukusanya pointi tisa ambapo itawakilisha kanda kwenye ngazi ya taifa kuwania safari ya kwenda Hispania kutembelea uwanja wa Camp Nou na kushuhudia michezo ya klabu ya Barcelona. (Picha: Executive Solutions)
 Nahodha wa timu ya Schalka 04 ya Dodoma Mussa Gaidi akiwa na wachezaji wenzake wakifurahi kutwaa ubingwa wa kanda ya Kati wa mashindano ya Castle Lager Perfect Six baada ya kushika nafasi ya kwanza kutoka kanda ya Kati katika michezo iliyofanyika uwanja wa Fire manispaa ya Morogoro kwa kukusanya pointi tisa ambapo itawakilisha michezo ya ngazi ya taifa kuwania safari ya kwenda Hispania kutembelea uwanja wa Camp Nou na kushuhudia michezo ya klabu ya Barcelona. (Picha: Executive Solutions)
 Mshabuliaji Ibrahim Nyagawa (Chuji) wa Schalke 04 ya Dodoma akikokota mpira wakati wa fainali za Kanda ya Kati hizo Morogoro.
Issa Kandula wa Mzinga FC na Delta Thomas wa Ndezi FC wakipambana kwenye fainali za Castle Lager Perfect Six kanda ya ya kati huko Morogoro wikendi hii.
Na Mwandishi wetu.

Kanda ya Kati imekuwa ya kwanza kupata wawakilishi kwenye fainali za mashindano mapya ya soka ya Castle Lager Perfect Six baada ya timu ya Schalke 04 ya Dodoma kutwaa ubingwa wa kanda hiyo katika fainali za kanda hiyo zilizopigwa kwenye uwanja wa Fire manispaa ya Morogoro wikendi hii.

Ubingwa huo kwa timu ya Schalke 04 inatoa nafasi ya kuwa mwakilishi kutoka kanda ya Kati kugombea nafasi ya kwenda nchini Hispania kutembelea uwanja wa Camp Nou na kushuhudia michezo ya klabu ya Barcelona katika La Liga endapo itashika nafasi ya kwanza katika michezo ya fainali ya ngazi ya taifa ya mashindano hayo yatayofanyika jijini Dar es Salaam siku za baadaye baada ya kupata mabingwa kutoka kanda saba.

Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili mjini Morogoro, Meneja wa Bia ya Castle, Kabula Nshimo alisema kuwa katika michezo ya ligi ndogo ya kanda ya kati ilikuwa na ushindani mkali kutokana na kila timu kujiandaa kushinda na kuibuka mabingwa katika kanda hiyo ambapo Schalke 04 ndiyo mabingwa wa kihistoria katika kanda ya kati.

Nshimo alisema kuwa Schalke 04 ilifanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwa kushinda michezo yake mitatu na kujikusanyia pointi tisa huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Mzinga FC ya Morogoro iliyopata pointi sita wakati Ndezi FC ya Morogoro imekusanya pointi tatu na kushika nafasi ya tatu na Market FC ya Dodoma ikiishia kupoteza michezo yote.

Nshimo alisema kuwa mechi zilizochezwa wikendi hii zimeonyesha jinsi gani Watanzania wana mwamko na shauku kubwa ya kushiriki mashindano kutokana na watu kujitokeza kwa wingi maeneo mbalimbali ambapo yalifanyika mashindano hayo ya kwanza.

Nshimo alisema mashindano ya Castle Lager Perfect Six yamelenga kuzungumza na wanywaji wa Castle Lager ambao wana shauku ya kucheza mpira wa miguu, kuleta pamoja wanywaji wa Castle Lager kutoka sehemu mbalimbali nchini ili wafurahie pamoja na kuwapa zawadi wateja hao wa bia hiyo.
Vilevile wikendi hii yalifanyika mashindano hayo kwenye mkoa wa Arusha na

Kahama katika hatua za awali kupata wawakilishi watakaocheza fainali za Kanda husika na pia zilifanyika fainali mkoa wa Temeke katika hatua za kupata wawakilishi wa Kanda kwenye fainali za taifa. Mashindano ngazi ya fainali za Kanda yataendelea wikendi ijayo kwenye mikoa ya Mwanza na Ilala na hatua ya kufuzu kucheza fainali za kanda itafanyika Moshi, Mbeya na Kinondoni.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: