7Baadhi ya wananchi wakipiga picha wakati tanki la mafuta la kampuni ya B. Clarke Haulege Construction, mali ya Bw. Bundala Kapela wa Igunga ni namba za usajili T634 BCZ llenye uwezo wa kubeba lita 40.000 za mafuta ya Petroli lililolipuka majira ya Saa 11:00 asbh katika barabara kuu ya Dodoma Mwanza eneo la Shelui mkoani Singida wakati breki za tanki hilo upande wa kushoto zilipojam na kusababisha moto. Jambo lilimfanya dereva wa roli lenye namba za usajili T 164 CGF aina ya Scania lililokuwa likivuta tanki hilo kusimamisha na kukata haraka tanki hilo huku akiondoa haraka injini ili kuepusha madhara zaidi ambayo yangeweza kutokea.

Katika tukio hilo lililosababisha usumbufu mkubwa kwa abiria na msururu wa magari kushindwa kupita katika eneo la ajali kutokana na moto mkubwa uliochanganyika na moshi, hata hivyo baada ya moto kupungua kiasi askari wa usalama barabarani waliamuru magari yaanze kupitia pembeni mwa barabara ili kuendelea. Hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa katika tukio hilo. (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-SHELUI-SINGIDA) 5 4 3 2 111Msururu wa magari ukiwa mkubwa katika eneo hilo baada ya kushindwa kupita kutokana na moto mkubwa.10Wananchi na wasafiri mbalimbali wakitoka kuangalia tukio hilo. 8Askari wa usalama barabarani akihakikisha mambo yanakwenda sawa ikiwa na kuangalia usalama unaimarishwa katika eneo hilo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: