Msemaji wa Kampuni ya PR Promotion, Victor Mkumbo (Kushoto) akizungumza mbele ya waandishi wa habari katika utambulisho wa Miss Mbagala 2014. Pembeni ni Mratibu wa Shindani hilo, Tesha Japhet (kati) na Meneja wa Kampuni ya Kampuni ya PR Promotion, Gervas Sinsahale.
Baadhi ya washiriki wa Shindano la Redds Miss Mbagala 2014 wakiwa katika picha ya pamoja.
---
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

Kampuni ya PR Promotion inawaletea Kitongoji kipya katika mashindano ya Urembo Tanzania kupitia wilaya ya Temeke ambayo ni Miss Mbagala 2014.

Miss Mbagala 2014 itajumuisha washiriki 16 kutoka maeneo mbalimbali ya Mbagala ambao ni Amina Salim (20), Aquilina Paul (22), Restuta Charles (21), Suzan Paul (19), Natalia Rogath (22), Grace John (20), Neema Roman (19), Lucrecia Mushi (20), Subira Ally (23), Lucy Lyombo (20), Joyce Mkandila (20), Lulu Baraka (22), Macklina Robert (21), Sylivia Robert (24), Esther Mnahi (20), na Maureen Msangi (20). 

Warembo wote watatambulishwa rasmi siku ya ijumaa tarehe 9/5/2014 sambamba na uzinduzi rasmi wa Miss Mbagala 2014 katika ukumbi wa Dar Live kuanzia saa 2 usiku Mbagala jijini Dar es Salaam.

Hii ni mara ya kwanza kitongoji cha Mbagala kuandaa mashindano ya Miss Tanzania baada ya kuongezwa na kamati ya Redds Miss Tanzania mwaka huu hivyo wilaya ya Temeke itakuwa na vitongoji vinne ambavyo ni Changombe, Kurasini, Kigamboni na Mbagala.

Washindi watatu wa mwanzo watashiriki moja kwa moja katika mashindano ya Redds Miss Temeke 2014.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: