Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kutoa heshima za mwisho kwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania Marehemu Flossy Gomile-Chidyaonga leo katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho kwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania Marehemu Flossy Gomile-Chidyaonga leo katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pole kwa wanafamilia na maafisa wa ubalozi wa Malawi alipokwenda kutoa heshima za mwisho kwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania Marehemu Flossy Gomile-Chidyaonga leo katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Balozi Frossie Chiyaonga, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Mei 12, 2014. Mwili huo unatarajia kusafirishwa kuelekea Malawi kwa maziko.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa Marehemu, Frossie Chiyaonga, aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania, aliyefariki ghafla Ijumaa ya wiki iliyopita, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Mei 12, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji baadhi ya wanandugu na familia ya aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Balozi Frossie Chiyaonga, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Mei 12, 2014. 
Sehemu ya waombolezaji waliojitokeza kwenye shughuli hiyo ya kuagwa mwili wa marehemu. PICHA ZOTE NA IKULU, OMR
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: