Bibi Sarah Kibonde Msika akitoa majibu ya Ufafanuzi kwa wanasemina.
Koplo Kelema akitoa kilio chake mbele ya Maafisa wa SSRA.Moja ya walimu wa TIA akitoa maelezo ya awali kabla ya Semina hiyo kunza.Wajumbe wa mkutano huo wakisikiliza kwa umakini.
---
Na: Atley Kuni- Afisa Habari Mwanza RS.

JESHI la POlisi mkoa wa Mwanza wamelalamikia kuhamishwa hamishwa kwenye mifuko ya hifadhi za jamii na kufanya michango yao mingine kutoonekana katika kuchangia kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.

Malalamiko hayo yalitolewa jana na baadhi polisi walioshiriki katik semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka ya usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii (SSRA) iliyohusu umuhimu wa kujiunga na mifuko ya hifadhi za jamii.

Akiongea kwa jazba katika semina, Martin Nkinga alisema wamekuwa wakihamishwa kutoka PSPF kwenda NSSF huku michango yao ikikwama njiani bila kufikishwa kwenye mfuko husika na hivyo kuwasabishia kero ya kufuatilia kila wakati bila mafanikio.

Wakati hayo yakijiri, Mfuko wa hifadhi ya Jamii wa (NSSF) na ule wa Bima ya Afya (NHIF) umezidi kuonyooshewa vidole na wadau wao mbele ya Mdhibiti na msimamizi wa mifuko ya hifadhi ya jamii katika semina za wadau zinazoendelea jijini humo

Wakiongea kwa uchungu askari Polisi hao Mwanza mbele ya Maafisa wa SSRA hapo jana wamesema,”’ ‘ NSSF imekuwa kero kubwa kwa wateja wake ikilinganishwa na mifuko mingine ya hifadhi ya jamii kwani mfuko huo mbali ya kuwa na Vitega uchumi vingi bado wanachama wao wameendelea kuwa wa hadhi ya chini zaidi”,alisena na kuongeza.

“Inashangaza kuona mtu umechangia sawa sawa na mwingine katika muda unaolingana kazini lakini mwisho wa kustaafu unakuta sisi wa NSSF tunapata mafao kiduuuchu sana ikilinganishwa na mwalimu au mtumishi mwingine aliyekuwa akichangia katika mifuko mingine” alisema mmoja wa polisi hao.

Huku Mkaguzi msaidizi wa Polisi Msangi yeye kiliochake aki kipeleka kwenye mfuku wa bima ya afya, (NHIF), kwamba hivi sasa wamekuwa na masharti magumu kwa wanachama kana kwamba matibabu wanayo yapata niya bure kumbe wanachangia mishahara yao, “Haiwezekani mtegemezi mtu amemuandika katika orodha ya wategemezi lakini inapofika wakati mtu huyo ameugua eti hatambuliki kwakuwa tuu jina lililokuwa kwenye kitambulisho na lile la muajiriwa havirandani wakati mimi nakatwa mshahara wangu tena bila yakuulizwa, huu ni unyanyasaji wa hali ya juu sana”.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa SSRA, bibi Sarah Kibonde Msika akitoa majibu kwa wadau hao alisema, “ Ni dhahiri kwamba zipo changa moto kadha wa kadha kwenye mifuko hii na sio rahisi kuzimaliza kwa wakati mmoja lililopo ni kwenda nazo taratibu na muda utafika, kama sio kuzimaliza basi tutazipunguza kwa kiwango kitakacho leta tija kwa wanachama.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: