Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA), mama Salma Kikwete (kulia) akizungumza na washiriki wa warsha ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono mara baada ya kukabidhiwa kitabu cha mwongozo wa namna ya kushughulikia mashauri mbalimbali ya kisheria alichokabidhiwa na Rais wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania Mh. Jaji Engera Kileo leo jijini Dar es salaam.
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA) mama Salma Kikwete akifungua warsha ya siku 1 ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono iliyoandaliwa na Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) leo jijini Dar es salaam.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA) mama Salma Kikwete (kushoto) akizungumza jambo na Bi. Salome Anyoti Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Jinsia, Usawa na Uwezeshaji wa Wanawake leo jijini Dar es salaam.
Washiriki wa warsha ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono wakiwa katika picha ya pamoja na mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) leo jijini Dar es salaam.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA), mama Salma Kikwete (kulia) akiagana na viongozi wa Chama Cha Majaji Wanawake Tanzania mara baada ya kufungua wa warsha ya siku 1 ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono.

Picha na Aron Msigwa - MAELEZO
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: