Timu ya Mpira wa pete (netball) ya wanahabari wa jijini Dar es Salaam, Taswa Queen juzi ilitwaa ushindi katika bonanza la nane la Waandishi mkoa wa Arusha, baada ya kuichapa timu ya chuo cha uandishi wa habari Arusha Arusha (AJTC) magoli 21-1.

Wakati Taswa Queen walikitwaa ubingwa kaka zao, TASWA SC , walishindwa kunyakuwa kombe, baada ya kutoka suluhu na timu ya AJTC katika mchezo mkali wa fainali, ambao ulisitishwa kutoka na kiza wakati wa mikwaju ya penati timu hizo, zikiwa zimefungana 1-1.

Kutokana na matokeo hayo, Meneja wa kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL), Endrew Warden alikabidhi Mwenyekiti wa Taswa SC Majuto Omar fedha taslim 200,000 na meneja wa AJTC Modaha Lucas alikabidhiwa kiasi cha sh 200,000.

Taswa SC, walifanikiwa kuingia fainali baada ya kuichapa timu ya Radio 5 magoli 3-1 na baadaye kuifungua timu ya Arusha 1-0 katika mchezo mkali wa nusu fainali.

Kwa Upande wa AJTC, waliingia fainali baada ya kuichapa timu ya Taswa Arusha, 1-0 na baadaye waliwatoa Sunrise radio kwa penati 11-12 baada ya timu hizo kutoka sale.

Katika mchezo wa fainali ya mpira wa pete uliochezwa uwanja wa general Tyre jijini Arusha, Taswa Queen iliicharaza Taswa Arusha 45-0 katika mchezo wa nusu fainali na kuisambaratisha AJTC ambao walikuwa mabingwa watetezi kwa mabao 53-1 katika mchezo wa fainali.
Kutokana na ushindi huo, Taswa Queen walikabidhiwa kikombe na Meneja mauzo wa kampuni ya Megatrade, Gudluck Kway na fedha taslimu 150,000.

Katika soka Taswa Dar pia ilifanikiwa kuingia fainali na timu ya AJTC na licha ya kupigiana mikwaju ya penati baada ya kutoka sare ya kutofungana, mshindi alishindwa kupatikana kutokana na kiza uwanjani.

Katika michezo mingine, timu ya ORS kutoka Manyara, ilifungwa na Sunrise 2-1 na baadaye ORS iliwafungua TBL Arusha goli 1-0 na hivyo kutwaa zawadi ya timu yenye nidhamu.

Katika tamasha hilo, katika mchezo wa kuku, wanahabari kutoka Taswa SC, AJTC na Taswa Arusha walitamba na kushinda.

Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary aliwapongeza wachezaji wake kwa ushindi huo huku akiwapongeza wadhamini wao, Delina Group of Companies, Said Salim Bakhresa & Co Ltd (Azam), DRFA na Kassim Dewji.
Tamasha hilo la nane la vyombo vya habari mkoa wa Arusha, liliandaliwa na TASWA Arusha kwa ushirikiano na kampuni ya Ms Unique na kudhaminiwa na TBL,TANAPA, Megatrade,AICC,Cocacola, Pepsi na Wazee Klabu.
 Baadhi ya wachezaji wa timu ya Taswa SC wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya bonanza la waandishi wa habari lililofanyika kwenye uwanja wa General Tyre, Arusha.

 Unaweza ukadhani kuwa ni wachezaji wa Azam FC, lakini hao ni kikosi cha kwanza cha 'mauaji' cha timu ya Waandishi wa Habari za Michezo nchini Taswa SC wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kupambana na timu ya Radio 5. Katika Mchezo huo uliofanyika kwenye viwanja vya General tyre mkoni Arusha, Taswa SC ilishinda kwa mabao 3-1

 Wachezaji wa timu ya Taswa SC wakipasha moto mwili kabla ya kuingia uwanjani katika uwanja wa General Tyre mkoani Arusha Jumapili. Taswa SC ilicheza fainali na timu ya chuo cha uandishi wa habari cha Arusha (AJTC) na kushindwa kufungana katika mchezo wa fainali. Hata hivyo timu hizo zilishindwa kupigiana penati kutokana na giza na hivyo kugawana zawadi ya mshindi wa kwanza.
Mchezaji wa timu ya Taswa SC, Juma Pinto akituliza mpira uku akilindwa na mchezaji wa Triple A. katika mchezo huo uliofanyika kwenye viwanja vya General Tyre, mkoani Arusha, Taswa SC ilishinda kwa mabao 3-1.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: