Joshua Arap Sang' leo alisimama kujitetea kwamba mashtaka dhidi yake katika mahakama ya kimataifa ya ICC, ni dhuluma kubwa, na kwamba hakuhusika na upangaji wa machafuko baada ya uchaguzi. Sang' alisema uwajibikaji wake kama mtangazaji na imani yake ya dini haingemuezesha kutenda maovu, anayotuhumiwa na upande wa mashtaka. Katika siku ya pili ya kesi ya jinai inayomkabili Sang' na naibu Rais William Ruto, upande wa mashtaka ulisema utawasilisha mashahidi 22 ambao wataonyesha namna, ghasia hizo zilivyopangwa na waasisi wakuu, Ruto na Sang'
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: