Mwanadada anayefanya vizuri sana kwenye muziki na filamu, baby Madaha nyota yake imeendelea kung'aa baada ya kupata dili la uhakika la milioni 50 kutoka katika kampuni ya Candy n’ Candy Records Label ya jijini Nairobi iliyomsainisha mkataba msanii mwingine wa Tanzania Mr.Nice hivi karibuni.

Akizungumza na Kajunason Blog leo, Msanii huyo alisema anamshukuru Mungu kwa kumuwezesha kupata mkataba huo ambao utamfanya aendelee mbele zaidi na zaidi.

"Kiukweli ni jambo la kumshukuru sana Mungu maana yeye ndiye muweza wa mambo yote, sikutegemea kuona kila wakati mambo yangu yanaendelea kusonga mbele bila ya vikwazo vyovyote, nimepata mkataba wa Milioni 50, nimepangiwa nyumba na kupewa gari zuri," alisema Msanii Baby Madaha.

Kwa upande wake meneja wa msanii huyo Joe Kariuki alisema kuwa pamoja na kumpa mkataba huo wa million hamsini (50) pia wamempa gari ya kutembelea ya kisasa aina ya AUDI TT na tumempangishia nyumba nzuri Kijitonyama jijini Dar es salaam.

Pamoja na hayo meneja huyo wa Mr.Nice ambaye ndio mmiliki wa studio hiyo alisema kwa sasa wanataka kumuhamishia msanii huyo jijini Nairobi, Kenya kwa kipindi cha mwaka mmoja ili afanye nao kazi huko kwani wamegundua kuwa anakubalika sana nchini humo na wapenzi wa muziki.

Baby madaha ametua nchini kutokea Nairobi akiwa pamoja na meneja wake kwa ajili ya kuachia video ya wimbo wake wa kwanza aliofanya na Label hiyo uitwao (Summer Holiday) ambao umefanywa huko huko jijini Naironi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: