Wakiwa na nyuso za furaha, ni Bwana Mussa na Bi. Myoma (Nadine) wakitoka kanisani.
Bwana Harusi Mussa akiwa na mke wake Myoma (Nadine) Kapya mara baada ya kufunga ndoa yao takatifu katika kanisa la KKKT- Azania Front jijini Dar.
 Ilikuwa ni nderemo na vifijo.
Wakikabidhiwa vyeti vyao.
 Wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kumaliza zoezi la kufunga ndoa.
 Mtu chake, Mussa akiwa amekamatia mke wake Nadine.
 Picha ya pamoja na wachungaji.
Pongezi.
 Mzee Simbeye akiwapongeza bibi Harusi Myoma (Nadine) pamoja na msimamizi wake Pauline.
 Baba mzazi wa bibi Harusi, Balozi Kapya (kushoto) akimpongeza mshenga wa bwana harusi kwa kazi yake nzuri.
 Wasimamizi wakijiweka sawa kumlaki bibi harusi na bwana harusi.
Chereko chereko...
Wapambe nao hawakuwa nyuma.
 Bwana Harusi Mussa na Bi harusi Myoma (Nadine) wakijadiliana jambo.
Show love.
 Baada ya harusi sherehe iliendelea katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam na huko nderemo na vificho vilitanda.
 Kaka wa bibi harusi akitambulishwa.
 Wageni waalikwa...
 Mama mzaa chema akimpongeza binti yake kwa kufunga pingu za maisha.
 Balozi Kapya akiwa na mkewe wakati wa kutoa nasaha kwa watoto wao.
Sasa ni mwili mmoja, Bwana na Bibi Mussa.
 Ngoma ya Kinyamwezi akipamba moto, ambapo bibi harusi ni Mnyamwezi na bwana harusi ni Kmakonde.
 Picha ya pamoja na wazazi.
Kwaito limekolea...
 Mama mzaa chema akitamka zawadi kwa mwanae.
 
Mama akimpatia mwanae zawadi ya mkufu na hereni za dhahabu ambao alimvalisha.
 Pia mama alimpatia mwanae kitambaa cha kushona shati kwa mwanae wa kiume.

 Pongezi kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki... akiwemo Mkama ambaye alisoma na bwana harusi tokea wakiwa shule ya msingi.

Kajunason Blog inapenda kuwatakia maisha marefu katika ndoa yenu maana iliandikwa; Mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: