Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Barnaba Elias 'Barnaba Boy' akitumbuiza katika tamasha la Kili Music Tour lililofanyika juzi kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika Mjini Kigoma.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ben Paul akiimba sambamba na Alice katika tamasha la Kili Music Tour lililofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika Mjini Kigoma.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Naseeb Abdul ‘Diamond’ akifanya yake katika tamasha la Kili Music Tour lililofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika Mjini Kigoma.
Msanii wa Hip Hop nchini, Fared Kubanda ‘Fid Q’ akikamua katika tamasha la Kili Music Tour lililofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika Mjini Kigoma.
Msanii wa muziki nchini Judith Wambura ‘Lady Jaydee akitumbuiza kwenye tamasha la Kili Music Tour lililofanyika kwenye Uwanja Lake Tanganyika Mjini Kigoma.
Baadhi ya wasanii wa muziki nchini wakiwa pamoja na Meneja wa bia ya Kilimanjari, George Kavishe katika tamasha la Kili Music Tour lililofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika Mjini Kigoma.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini |Linex Sunday ‘Linex’ akilishambulia jukwaa kwenye tamasha la Kili Music Tour lililofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika Mjini Kigoma.
Msanmii wa muziki wa Hip Hop nchini Joseph Haule ‘Profesa Jay’ akitumbuiza katika tamasha la Kili Music Tour lililofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika Mjini Kigoma.
Msanii wa muziki nchini Rachel akicheza pamoja na mcheza shoo wake katika tamasha la Kili Music Tour lililofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika Mjini Kigoma.
Umati wa mashabiki waliojitokeza kwenye tamasha la Kili Music Tour, wakifuatilia onyesho hilo lililofanyioka kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika Mjini Kigoma.
---
Na Mwandishi Wetu

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul, juzi alifunia katika tamasha la Kili Music Tour lililofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika Mjini Kigoma.

Katika tamasha hilo lililohudhuriwa na umati mashabiki, Diamond alifanya onyesho la aina yake na kuwafanya mashabiki kumshangilia kwa kupiga kelele.

Msanii huyo alipanda jukwaani na kuanza kutumbuiza baadhi ya vibao ikiwa ni pamoja na Nimpende Nani, Moyo Wangu, Nataka Kulewa pamoja na Kesho.

Hata hivyo Diamond alionekana kuwakosha maelfu wa mashabiki baada ya kuanza kuimba wimbo wa Muziki Gani aliomshirikisha Ney wa Mitego na kuwafanya watu wamshangilie kwa kupiga kelele.

Diamond ambaye alikuwa msanii wa mwisho kupanda jukewaani, aliwaita wasanii wenzake ambao ndio wenyeji wa Kigoma kama Rachel, Mwasiti pamoja na Linex na kuimba wimbo wa Lekadutigite na kuwaamsha mashabiki waliofurika Uwanjani hapo.

Wasanii wengine ambao walitumbuiza katika onyesho hilo lenye ujumbe wa ‘Kikwetu Kwetu’ ilikuwa ni pamoja na Barnabas, Ben Paul,Izzo Business, Profesa Jay, Fid Q, Roma Mkatoliki pamoja na Kala Jeremiah.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: