Kundi la kwanza la wasanii watakaotumbuiza katika tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2013 limewasili mkoani Kigoma kwa ajili ya onyesho hilo. Wasanii hao 8 ni kati ya 12 watakaopanda katika jukwaa moja uwanja wa Lake Tanganyika siku ya Jumamosi. Kundi la pili la wasanii ambao ni Profesa Jay, Diamond, Lady Jaydee na Barnaba wanatarajiwa kuwasili siku ya Jumamosi asubuhi.

Baada ya kupata mlo wa mchana ulioandaliwa na mwenyeji wao ambaye ni Doctor Gerrard Mipango wasanii hao walipata nafasi ya kutembelea makumbusho ya Doctor Livingistone yaliyoko Ujiji na kujionea historia mbalimbali ya mzungu huyo anayetambuliwa kama mvumbuzi wa Ziwa Tanganyika na pia kuona maeneo biashara ya utumwa ilipokuwa ikifanyika na kujifunza kuhusu asili ya wenyeji wa Mkoa wa Kigoma.
Mwasiti, Ben Pol na Roma baada ya kutua uwanja wa ndege wa Kigoma
Fid Q, Kala Jeremiah na DJ Choka eneo la abiria waliowasili uwanja wa ndege
Fid Q akitoka nje ya uwanja wa ndege
Roma Mkatoliki akiondoka eneo la uwanja wa ndege
Recho akijielekeza kwenye usafiri kuelekea hotelini
Izzo Bizness akitoka uwanja wa ndege wa Kigoma
Mtoto wa Kigoma Linex alikuwa wa mwisho kutoka nje ya uwanja wa ndege wa Kigoma
Wasanii wakipata mlo wa mchana nyumbani kwa Askofu Gerrard Mipango mjini Kigoma
Wakali wa muziki katika picha ya pamoja na wenyeji wao mkoani Kigoma.
Wasanii wakiwa katika eneo la mbele ya makumbusho ya Doctor Livingstone
Roma Mkatoliki akisaini kitabu cha wageni kwa niaba ya wasanii wengine
Wasanii wakimsikiliza mtaalam wa historia ya makumbusho ya Doctor Livingstone
Mwasiti akisoma njia zilizotumika wakati wa biashara ya utumwa.
Mtaalam wa historia akiwaonyesha wasanii mavazi ya wenyeji wa zamani wa mji wa Ujiji
Fid Q kama anajaribu kuwapatanisha Dr Livingstone na mwenzake.
Baada ya kufanya ziara wasanii walipata nafasi ya kufanya manunuzi katika soko la Kigoma
Wakazi wa Kigoma wakiwaangalia wasanii wakati wakifanya manunuzi soko kuu la Kigoma
Muuzaji viatu akiwakaribisha wakali wa muziki kuangalia mzigo
Mashabiki hawa hawakutaka kupoteza nafasi ya kuonyesha upendo kwa Fid Q
Wasanii wakirejea kwenye basi lao ambalo lilikuwa limezongwa na mashabiki
Mwasiti katika picha ya pamoja na mashabiki waliomuomba
"Konda" wa basi la wasanii Mwasiti akifunga mlango kwa ajili ya kurejea hotelini walikofikia.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: