Kundi la kinadada watatu linalofanya vizuri kwenye tasnia ya muziki Tanzania,The TRIO, leo wametoa wimbo wao mpya unaoitwa, ‘FALL IN LOVE’.
Kundi hilo ambalo limekuwa kwenye muziki kwa muda mrefu kidogo, limetoa wimbo huu kama ujio wao mpya, baada ya wimbo wao wa kwanza ‘PAMBO’ kupata mafanikio makubwa.
Kundi hilo pia ambalo mmoja wa washiriki wake, Malaika, anawania tuzo za Kili kama mmoja wa wasanii wanaochipukia baada ya kufanya vizuri kwenye wimbo wa Ommy Dimpoz, Baadae, wamesema wimbo huu utawashika sana mashabiki wao.
‘Tunaamini wimbo huu utafanya vizuri sana, kwani tumeuandaa kwa muda mrefu, na tumezingatia mahitaji ya mashabiki wetu’ walisema.
Kundi hilo linaundwa na kinadada watatu machachari, Angella Karashani (Malaika), Alice Kibopile (Alice) na Khadija Maige (Kadja)
Wimbo umerekodiwa studio ya Sourround Sound, chini ya mtayarishaji Ema The Boy.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: