Na Mwandishi Wetu

MAZOEZI kwa ajili ya kujiandaa na shindano la kumsaka malkia wa Mkoa wa Tanga mwaka huu "Redd's Miss Tanga 2013" yanaanza leo kwenye Ukumbi wa Lavida uliopo jijini Tanga.

Akizungumza na blog hii, Mkurugezi wa Kampuni ya DATK Internmediate, Asha Kigundula, alisema kuwa maandalizi ya shindano hilo yanaendelea vizuri.

Kigundula alisema kuwa walimu watakaosimamia warembo hao ni Miss Tanga 2012 Teresia Kimolo na Mwanaid Omar.

Alisema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri, ambapo warembo wameanza kuitikia wito wa kushirikishi shindano hilo.

Kigundula alisema kuwa mpaka sasa jumla ya warembo 8 wamejitokeza kushiriki shindano hilo ambapo nafasi bado iko wazi kwa wasichana wote wenye sifa za kushiriki.

"Kila kitu kinaendelea vizuri, ikiwa na warembo kuendelea kujiandikisha kushiriki shindano la mwaka huu, ambalo nina hakika litakuwa la aina yake"alisema Kigundula

Alisema kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo mkoani humo kwa kuwa Kampuni DATK imejipanga, hivyo mashabiki wa mashindano ya urembo wa jijini hapo kwa ujumla wakae mkao wa kupata raha.

Pia alisema fomu zinapatika katika ofisi ya Mwananchi iliyopo Bandari Tanga ghorofa ya Nne, Five Brathers kwa Nassa Makau iliyopo jijini humo, kwa Dar es Salaam zinapatikana katika ofisi za Jambo Leo zilizopo Jengo la Hifadhi Hause Posta.

Redd's Miss Tanga 2013, imedhaminiwa na CXC Africa, Tanga Beach Resorts, Lavida Pub, Jambo Leo, Staa Spoti, Clouds Media Group, pamoja na  Michuzi Media Group, Bongostaz.com, Saluti5, Kajunason Blog, JaneJohn, na Kidevu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: