Mwili
wa dereva wa lori moja kubwa lenye ujazo wa tani 18 ukiwa umeopolewa na
askari jeshi, tayari kupelekwa mochwari ya Hospitali ya Mt Meru. Dereva
huyu ametambulika kwa jina moja tu la Alex amefikwa na mauti akiwa
ndani ya gari hilo wakati vijana wengine wakiendelea kupakia moram
asubuhi ya leo
Baadhi
ya wananchi waliojitokeza kushuhudia ajali hiyo mbaya wakishangaa zoezi
la uokoaji na wengine wakisubiri kutambua ndugu zao, jambo ambalo
halikupata nafasi.
Mwananchi huyu aliishiwa nguvu baada ya kushuhudia mwili wa rafiki yake ukiopolewa kutoka kwenye kifusi
---
Inakadiliwa watu zaidi ya watu 18 wamepoteza maisha kufuatia
kufukiwa na gema la mchanga/moram wakati wakichimba na kupakia kwenye
malori eneo la Moshono jijini Arusha.
Ajali hiyo mbaya imetokea katika machimbo ya moram nje
kidogo ya jiji eneo jirani na Moshono-Kiserian ambapo vijana hao
wanaokadiriwa kufikia idadi hiyo walikuwa wakipakia moram kwenye magari
mawili, moja ni Fuso na lingine kubwa zaidi (tani 18) na yote mawili
yamefukiwa kabisa na kifusi.
Shuhuda mmoja wa ajali ambae pia ni
mchimbaji ameieleza Blog hii kwamba kwa kawaida gari ndogo kama Fuso
hupakiwa na watu 7, na hiyo kubwa huwa na watu 12 bila kuhesabu dereva
na utingo.
Miongoni wa waliofikwa na mauti ni pamoja na madereva wa
magari hayo.
Katika eneo la ajali hali ni ya simanzi na vilio
toka kwa kina mama huku baadhi wa wababa na marafiki na ndugu wa jamaa
waliofukiwa wakishindwa kujizuia na kuangua kilio.
Meya wa
Manispaa Mh Gaudence Lyimo pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless
Lema ni miongoni mwa viongozi wakubwa waliofika eneo la ajali kusaidiana
na kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania kufanya uokozi.
Wachina wakipeleka moja ya mashine zao (Excavator)
kuongeza nguvu katika kusaidia kufukua miili ya watu hao iliyonaswa na
kifusi hicho.
HABARI KWA HISANI: ARUSHA255 BLOG
Toa Maoni Yako:
0 comments: