Mshindi wa promosheni ya Ascend Y200 Fred Mgaya aliyejishindia zawadi ya kugharamiwa na Tigo gharama zote za kutembelea miji mikubwa nchini China akiwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa JK Nyerere leo.

Promosheni ya Tigo ya Ascend Y200 ilizinduliwa rasmi mnamo mwezi Oktoba mwaka 2012 ambayo inamuwezesha mteja kununua smartphone yenye kiwango na hadhi ya juu aina ya 'Ascend Y200' kwa punguzo la hali ya juu.

Jumla ya washindi wawili walipatikana ambao ni Bw. Fred Mgaya mwanafunzi wa KCMC Moshi na Bw. Simon Richard mkazi wa Ubungo Dar es Salaam, washindi hao walitembelea vivutio mbalimbali kwa nusu siku jijini Guangzhou na mapumziko ya siku nzima katika milima ya Lotus nchini humo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: