Aliyewahi kuwa Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006 Jokate Mwegelo alijitolea kuwafungulia website kikundi hicho ili kiweze kujitangaza na kutambulika ndani na nje ya nchi.
Jokate alisema kuwa ili kikundi hicho kifanikiwe ni lazima wajitambue na kuwe na timu imara ambayo itakuwa makini na nia thabiti ya kujiinua kimaisha na kukuza uchumi wa Taifa.
"Mafanikio niliyokuwa nayo si kwasababu mimi ni bilionea bali ni kutokana na ushirikiano tuliokuwa nao mimi na wenzangu hadi tukafanikiwa kuwa na kampuni inayojulikana kama kidoti". Alisema Jokate.
Aliongeza kuwa japo kuwa wanakabiliana na changamoto mbalimbali lakini wanaendelea vizuri na biashara ambapo mbali na kuuza nywele tunatarajia kuuza vipodozi pamoja na nguo
Mbali na hilo alisema kuwa ili wafanikiwe ni lazima wawe na upendo ili kila mtu aweze kuwa huru na kueleza kile anachokiona kina manufaa katika kikundi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: