Bi Kidude enzi za uhai wake

Na Waandishi Wetu

MWIMBAJI mkongwe wa taarab, Fatma Baraka maarufu kama Bi Kidude amefariki dunia muda huu.

Mjukuu wa marehemu, Fatuma Kidude amekaririwa kutoka Zanzibar, akisema bibi yake amefariki nyumbani kwa mtoto wa kaka yake maeneo ya Bububu.

Fatma ambaye naye pia ni mwimbaji, akiimbia kundi la Gusa Gusa la Dar es Salaam ameongeza kuwa bado taratibu za mazishi zinaendelea kufanyika lakini mwili wa marehemu unahamishwa muda huu kupelekwa nyumbani kwake Raha Leo.

Mara kadhaa kumewahi kutokea uzushi wa Bi Kidude kufariki, lakinikwa sasa habari hizi ni sahihi kwa aslimia mia moja. Bi Kidude alianza kusumbuliwa na mapema mwaka jana, lakini baadaye akapata ahueni na kufanya mahojiano hadi na vyombo vya habari, lakini ghafla mambo yakabadilika tena na kulazwa katika hospitali ya Hindu Mandal, Dar es Salaam.

Fatuma binti Baraka au Bi Kidude, alizaliwa katika kijiji cha Mfagimarigo Zanzibar katika familia ya watoto saba (7). Baba yake Mzee Baraka alikuwa ni mfanyabiashara wa nazi, zao ambalo ni la kutumainiwa sana Zanzibar.

Bi Kidude aliwahi kusema enzi za uhai wake kwamba hafahamu tarehe halisi aliyozaliwa, isipokuwa alichokuwa anajua ni kwamba alizaliwa wakati rupia ikitumika kama fedha, na vilevile ana hakika ni kabla ya Vita Kuu ya Kwanza ya Ulaya.
Mmiliki wa mtandao huu wa Kajunason Blog (Cathbert Angelo) akiwa na Bi Kidude enzi za uhai wake.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: