*MTANGAZAJI ANAPOAMINI KUWA “AMETISHA VYA KUTOSHA”

Kuna mtangazaji mmoja kijana tu, umri miaka 22 (jina ninalihifadhi) ameniandikia email hii;

“Mimi ninafanya vipindi vya burudani wakati wa weekend, kwenye redio....... na japo ninajikubali na kipindi changu kinakubalika ninahisi kwamba nimetisha vya kutosha kwenye redio hii, kwa maana sioni jipya, je? Ni hisia tu au labda mazingira ya kazi yananiboa kwani naona hamna jipya? Au labda nahitaji kujifunza mambo mapya au kutafuta kazi kwenye redio kubwa kubwa za huko Dar?"

MENEJA VIPINDI WA REDIO CLOUDS FM, SEBASTIAN MAGANGA (PICHANI): USHAURI WANGU KWAKE, NA KWAKO KAMA UNAPITIA HALI HII:

SHERIA YANGU NAMBA MOJA KWA WATANGAZAJI NI HII.. UKIHISI IMEFIKIA HATUA AMBAPO HUWEZI KUONGEZA AU KUJIFUNZA CHOCHOTE KWENYE KITUO CHAKO, AU HATA WAFANYAKAZI WENZAKO, UNAHITAJI KUANZA KUFIKIRIA NAMNA YA KUTOKA KATIKA HATUA ULIOPO.

KAMA ILIVYO KWA FANI AU TAALUMA YEYOTE, KAMA HAKUNA CHANGAMOTO, AU FURSA YA KUONGEZA VITU VIPYA, INAWEZA IKAKUFANYA KUSHINDWA KUHAMASIKA NA IKAATHIRI UTENDAJI WAKO, WA KILA SIKU, AU HILO LIKISHINDIKANA (LA KUPATA KAZI KWENYE KITUO KINGINE HUSUSANI VYA DAR ULIVYOPENDEKEZA) SI MBAYA KUANZA KUTAFUTA HAMASA YA KILE UNACHOFANYA NJE YA MAZINGIRA YA STUDIO, TENGENEZA UTARATIBU WA KUTEMBELEA MITAA MBALIMBALI TOFAUTI NA SEHEMU UNAZOENDA KILA WAKATI, UPATE MAWAZO NA HADITHI ZA WATU MBALIMBALI, SIKILIZA REDIO AU TAZAMA TV ZA NJE YA MAZINGIRA YAKO NA UCHUKUE BAADHI YA VITU NA KUVIONGEZEA UBUNIFU WAKO ILI VIENDE SAMBAMBA NA MSIKILIZAJI WAKO, JIFUNZE JAMBO MOJA AU MAWILI KUTOKA KWENYE MAGAZETI KILA UKISOMA, NA ZAIDI TEMBELEA BLOGS, SITES NA MTANDAO KIUJUMLA, NA KUTUMIA VITU VILIVYOPO HUKO KWA FAIDA YAKO, KWANI KADIRI UNAVYOPANUA UBONGO WAKO NDIVYO UNAVYOJIFUNZA VITU VINGI NA HIYO INAONGEZA HAMASA YAKO.

KIFO CHA MTANGAZAJI YEYOTE, NI PALE AMBAPO ANAAMINI KUWA ETI “AMETISHA VYA KUTOSHA”.

Kama unalolote wasiliana nami: sebastianmaganga@gmail.com
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: