Meneja wa Tigo Pesa Bi. Catherine Rutenge Alisema “dhumuni kuu la kubadili bei na kuweka viwango vipya ni kuhakikisha kuwa wateja wa vipato vyote hususan wenye vipato vya chini wanaweza pia kunufaika na huduma zetu",
Kampuni ya Tigo pia imedhihirisha kuwa imepunguza bei za kutuma pesa kutoka kwa wateja waliosajiliwa na Tigo Pesa kwenda kwa wateja wasiosajiliwa na wale wa mitandao mingine, hivyo kurahisisha zoezi la utumaji hili na kulifanya la bei nafuu kabisa.
Pamoja na mabadiliko ya bei, Tigo Pesa imezindua promosheni ya ulipaji bili ambapo wateja waliosajiliwa na Tigo Pesa wanapolipa bili zao za Luku, Star-times, Zuku, Dawasco, au DSTV, wanazawadiwa kiwango cha Tshs 1,000 cha salio la kupiga simu siku inayofuata. Nyongeza hii inaweza kutumika ndani ya siku mbili kwenye kutuma SMS kutoka Tigo kwenda Tigo, au kutoka Tigo kwenda mitandao mingine yote hapa nchini.
Vilevile sasa unaweza kutuma kiasi cha fedha kuanzia shilingi mia mbili (200) mpaka shilingi milioni moja (1,000,000) kupitia Tigo Pesa.
“Tigo inataka kuhakikisha kuwa wateja wake wana nafasi ya kuchagua huduma na bidhaa mbalimbali . Tunataka kuwajumuisha watu wa aina zote kwenye kutumia huduma zetu. Tunaona jinsi watumiaji wa simu wanavyotegemea simu zao za mkononi kwa utatuzi wa mambo mbalimbali na hivyo basi tunahakikisha kuwa tuko mstari wa mbele kuwapa huduma bora zaidi na zenye unafuu.” Alimalizia Ndg. William Mpinga, meneja wa chapa ya Tigo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: