Tapeli aliyefahamika kwa jina la Rashidi Hussein (27), Mkazi wa Shule ya Msingi Kigogo 'C' leo jioni amepokea kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali baada ya kukamatwa akitaka kumtapeli kiasi cha tsh. 500,000/- kutoka kwa mama mmoja ambaye anaendesha biashara yake ya M-Pesa eneo Kijitonyama Sokoni jijini Dar es Salaam.
Akisimulia mkasa huo mama huyo ambaye hakupenda jina lake litajwe, alisema kuwa majira ya saa 11 kasoro jioni walifika vijana wapatao watatu ambao walikuja kwa nia ya kuwekewa pesa kiasi cha tsh. 5,000/- ndipo mama huyo alipompa simu ili aandike namba yake tapeli Rashidi Hussein, aliandika namba na kumbeep mwenzake kwa siri ili apate namba ya mama huyo na yeye alihihifadhi kwa siri namba ya rafiki yake kwenye simu ya mama huyo kwa jina la M-Pesa.
Mama huyo alioona tapeli Rashidi anachukua muda mrefu kuandika namba yake kwenye simu ndipo alipoamua kumnyang'anya simu ile na kukuta amehifadhi namba yake kwa jina la M-Pesa. Alipoona kuwa tapeli Rashidi amehifadhi namba yake alichukua jukumu la kuiandika namba ile kwenye karatasi na kuifuta kwenye simu yake na hapo ndipo akishtuka kuwa kuna mchezo anataka kuchezewa.
Aongeza kuwa baada ya kuwa amemaliza kumhudumia tapeli Rashidi kwa kumuwekea tsh. 5,000/- katika simu yake. Tapeli Rashidi aliondoka lakini baada ya muda mfupi alirejea na kumuuliza mama huyo kuwa amerudi kutoa pesa kwenye M-Pesa kiasi cha tsh. 500,000/-, alimjibu sawa na hapo ndipo alipompigia simu aliyedai ni Mjomba wake kwa kumwambia tuma basi hiyo hela.
Mama huyo anasema, wenzake ambaye mara ya kwanza aliwabeep namba ya yake alituma mesaji ya uongo kwa mama yule na kuonyesha namba ya kawaida kuwa imetoa kiasi cha tsh. 500,000/- na hapo ndipo alipowaita vijana waliokuwa maeneo ya kibanda hicho na kuomba msaada na kufanikiwa kumkamata tapeli Rashidi na kuanza kumpa kichapo ili awaseme wenzake. Wenzake ambao walikuwa wakimsubiria pembeni baada ya kuona hayo alikimbia.
Mama huyo alishukuru kufuta namba ile maana bila ya kufuta mesaji ingeingia kwa jina la M-Pesa na kujikuta ametoa hela kiasi hicho cha tsh. 500,000/= na kumpatia tapeli Rashidi. Alitoa shukrani kwa majirani zake ambao walionyesha ushirikiano katika kumkamata tapeli huyo ambaye alikutwa na sim card za mitandao mingine pamoja na kitambulisho cha kupiga kura.
Pichani ni wananchi wakitoa kipigo kwa tapeli Rashidi.
Wananchi wakimwadabisha tapeli Rashidi Hussein (27), Mkazi wa Shule ya Msingi Kigogo 'C'(ambaye hajavaa shati.
Tapeli Rashidi Hussein (27), Mkazi wa Shule ya Msingi Kigogo 'C'akijitetea mbele ya wananchi wenye hasira kali.
Kila mmoja akiwa na hamu ya kutoa kichapo kwa tapeli Rashidi Hussein ambaye alikamatwa na mama mwenye kibanda cha M-Pesa.
Tapeli Rashidi Hussein (27), Mkazi wa Shule ya Msingi Kigogo 'C' akilia huku pembeni yake kukiwa na sim card nyingi ambazo alikuwa akitumia kufanya utapeli huo.
Wananchi wenye hasira kali wakitoa kichapo kwa tapeli Rashidi Hussein.
Tapeli Rashidi Hussein (27), akimwagika damu baada ya kichapo hicho.
Wananchi wakishauliana kumpeleka polisi baada ya kumpa kichapo, huku wengine wakikataa na kusema haina haja ni bora wamuue jambo lililopigwa na wengine.
Akivushwa barabarani kupelekwa kituo cha polisi mabatini jijini Dar.
Baada ya kuvushwa barabara tapeli huyu alitaka kukimbia ndipo alipopigiwa mayowe ya mwizi na kumfanya asimame.
Msafara wa kwenda polisi.
Mama mwenye kibanda cha M-Pesa (aliyejishika kiuno) alinusurika kutapeliwa baada ya kumshitukia tapeli huyo.
Mama akiwa katika hali ya mshangao baada ya kunusurika kutapeliwa kiasi cha tsh. 500,000/-
Hiki ndicho kitambulisho cha tapeli huyo mara baada ya kusachiwa na kukutwa na sim card nyingi za mitandao tofauti tofauti.
Toa Maoni Yako:
0 comments: