Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma David Misime akiongea katika mkutano na vyombo vya habari wakati akielezea tukio la kuuwawa kwa majangili hao.

Habari/Picha na John Banda, Dodoma

MAJANGILI watatu wa nyara za serikali wameuawa kwa mishale yenye sumu na kisha miili yao kuchomwa moto na wananchi katika purukushani na polisi walipokuwa wakijaribu kukimbia ili kutorosha meno ya tembo.

Tukio hilo lilitokea jioni ya alhamis wiki hii katika kijiji cha Miganga kata ya Mvumi wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma ambapo miili yao ilikutwa ikiwa imehalibika kutokana na kuchomwa moto.
Mwili wa Jangili ukiwa umeharibika baada ya kuuawa kwa kuchinjwa na kuchomwa moto. Miili yote imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Mvumi Dodoma.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, David Misime alisema majangili hayo yaliuawa na wanachi wenye hasira kali kwa zana mbalimbali za kijadi walipokuwa wanakimbilia porini ili kujiokoa na mkono wa polisi.

Misime alisema jeshi hilo alipokea taarifa kutoka kwa wananchi wema kuwa kulikuwa na Gari likitokea Manda likiwa na Meno ya Tembo na kisha kuweka mtego katika kijiji cha Mwitikila ambapo waliona gari aina ya NOAH T 983 BZJ na kulisimamisha na Dereva wa Gali hilo alifanya kama anapunguza mwendo na kisha kuondoka kwa mwendo wa kasi.
 Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma David Misime akiwaonyesha waandishi wa Habari meno 73 ya tembo yenye thamani ya zaidi 225 mil ambayo ni sawa na tembo 36 pamoja na Gari aina ya Noah NO T 983 BZJ waliokamata juzi katika kijiji cha Miganga mvimi wilayani Chamwino Dodoma.

‘’Polisi wakishirikiana na wananchi walianza kulifukuza walipofika kijiji cha Miganga Mvumi polisi walifanikiwa kupiga Risasi tairi moja ya kushoto na hivyo watu watatu waliokuwemo ndani gari hilo waliruka na kutawanyika, wananchi waliojichukulia sheria mkononi waliwashambulia kiasi cha kupoteza maisha yao’’, alisema

Aidha kamanda Misime alisema baada ya kulipekua Gari hilo walikutaMeno 73 ya Tembo yenye uzito wa kilo 255.9 yakiwa na thamani ya zaidi ya Tsh Mil. 225 pamoja na hati ya mashitaka [CHARGE SHEET] ambayo ni kesi ya kuhujumu uchumi namba 4/2012 iliyokuwa imefunguliwa katika mahama ya Mpanda mkoa wa Katavi na Leseni ya Udereva na 4000692535 Aboubakar Peter huku wakihisi ni mmoja ya waliouawa.

Alisema walikuwa wameshitakiwa kwa kosa la kupatikana na Meno 3 ya Tembo Tarehe 17.06.2012 na maafisa wanyama pori katika eneo la Msaginya Wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi majina ya walikuwa wameshatakiwa ni Joseph Marius [NGONDO] 59 mkazi wa maili mbili Dodoma, Aboubakar Mhina 25 mkazi wa Mkuhungu Dodoma, Msafiri Milawa 36 mkazi wa Nkuhungu Dodoma na Petro Mtipula 55 mkazi wa mpanda.
Miili ya watu waliodhaniwa kuwa ni Majangili ikiwa imeharibika baada ya kuuawa kwa kuchinjwa na kuchomwa moto ikiwa imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti mvumi Dodoma.

Kamanda alitoa wito kwa wananchi wasijichukulie Sheria mikononi kwani kwa kufanya hivyo ni kupoteza ushahidi na inawawia vigumu polisi kupata mtandao inayohusika na matukio kama hayo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: