Padri Evaristitus Mushi wa Kanisa katoliki, Parokia ya St. Joseph, Shangani, Unguja amepigwa risasi ya kichwa na kufariki dunia majira ya saa 1:30 asubuhi na watu wawili wasiofahamika ambao walikuwa wamepanda piki piki aina ya Vesper katika eneo la Beit-EL-Ras karibu na kanisa la Katoliki.

Kajunason Blog ilifanya mahojiano na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Zanzibar, Inspekta Mohammed Mhina ambaye alidhibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema kuwa Padre huyo ameuwawa wakati akijiandaa kuingia kanisani akitokea kwenye gari yake ambapo ghafla ndipo alipopatwa na umauti.

Inspekta Mhina amelaani kitendo cha kuuwawa kwa lPadre huyo na kusisitiza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na msako ili kuweza kuwabaini wauaji.

Hili ni tukio la pili kutokea ambapo tukio la kwanza lilitokea kwa Padre Ambrose kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

1 comments:

  1. Mungu uilaze roho ya padre mushi mahali pema amina

    ReplyDelete