Kanisa katoliki nchini limetoa tamko kufuatia kifo cha Padri Evaristus Mushi, ambapo limewataka waumini wa kanisa hilo popote walipo kuwa watulivu na kufanya maombi ya amani kwa nchi katika kipindi hiki cha maombolezo.

Askofu mkuu wa kanisa katoliki nchini Muadhama Polycup Cardinal Pengo amesema kifo cha Padre Mushi ni pigo kwa kanisa na Taifa kwa ujumla na ni ishara ya kutoweka kwa amani hivyo suala hilo linapaswa kufanyiwa kazi mapema kabla halijasababisha madhara zaidi kwa nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Cardinal Pengo amevitaka vyombo vya usalama kufanya uchunguzi wa kina ili kuwatia mbaroni wote waliohusika na mauaji hayo.

Cardinal Pengo  amesema viongozi mbalimbali wa kanisa katoliki wataungana na waumini wengine February 20 mwaka huu katika mazishi ya Padre Mushi huko Zanzibar huku misa kubwa ya kuomba amani ikipangwa kufanyika siku hiyo katika kanisa katoliki la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

1 comments:

  1. Tuombe Mungu kwa watu wote wanaopenda amani, viongozi wa nchi wanapaswa kuzingatia hali ya usalama kwa nchi na raia wake kwa ujumla, Mungu aiweke roho ya marehemu peponi, Raha ya milele umpe ee bwana na mwanga wa milele umuangazie apumzike kwa amani. AMINA

    ReplyDelete