Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Rick Ross akiimba jukwaani  usiku huu mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake kwenye viwanja vya Lidaz Club,wakati wa tamasha la Serengeti Fiesta likirindima.
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti SBL Bw Ephraim Mafuru akitangaza mshindi wa bahati nasibu ya magari mawili kwa mkoa wa Dar es salaam iliyoendeshwa katika matamasha yote ya Serengeti Fiesta mwaka huu kutoka kulia ni Bw. Mrisho kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha , Rugambo Rodney Meneja masoko wa Push Mobile na kushoto ni Mkurugenzi wa Clouds Entarteinment Bw Joseph Kusaga wakishuhudia tukio hilo.Wadau kutoka Serengeti wakifyrahia jambo katika burudani ya muziki.

 Mkali mwingine wa miduara AT na madansa wake wakilishambulia jukwaa.

 Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT,akiimba jukwaani na shabiki wake.
 Mashabiki wakitaka kuangusha uzio uliowekwa kwa ajili ya usalama.
 Viwanja vya Lidaz palikuwa hapatoshi hata kidogo.
 Mwanamuziki kutoka nchini Marekani, Rick Ross akijisikia furahaa kuwaona Watanzania wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwa ajili ya kumshuhudia yeye akikamua stejini.
Msanii wa miondoko ya rusha rohoo a.k.a Miduara, Shilole akijiachia jukwaani vilivyo na madansa wake usiku huu mbele ya umati mkubwa uliofika kwenye viwanja vya Lidaz Club,katika kuhitimisha kilele cha tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: