Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania, Bi. Elizabeth Michael leo amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kujibu mashtaka yake ya kuhusika na kifo cha muigizaji mwenzake nguli nchini Marehemu Steven Kanumba. 

Elizabeth Michael amesomewa mashtaka hayo mbele ya hakimu Agustino Mmbando na wakili Elizabeth Kaganda ya mauaji ya Muigizaji wa Filamu nchini, Marehemu Steven Kanumba yaliyotokea huko Sinza Vatcan jijini Dar es Salaam april 7 mwaka huu.

Elizabeth Hakutakiwa kujibu chochote Mahakamani hapo kwani mahakama hii haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.

Kesi hiyo imeahirishwa na kupangwa kusikilizwa tena april 23 mwaka huu.

Muigizaji huyo aliletwa mahakamani hapo kwa mwendo wa kasi kama mshale na kwa ulinzi mkali na pia ndivyo alivyoondolewa Mahakamani hapo kiasi kwamba hakuna hata mwandishi alieweza kupata picha ya Muigizaji huyo mwenye tuhuma za mauaji Na kupandishwa katika gari ndogo nyeupe aina ya suzuki grand vitara yenye nambari za usajiri T 848 BNV huku kwenye kioo nambari zake zikisomeka PT 2565. 

Habari kwa Hisani ya Blasio Kachuchu wa Kajunason Blog.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: