*Ataka Wakuu wa Mikoa wawasimamie Wakurugenzi wa Halmashauri
*Asema watakaokiuka magizo ya CAG kuvuliwa madaraka

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema masuala ya ugavi na manunuzi bado yanakabiliwa na changamoto nyingi na kwamba usimamizi zaidi unahitajika ili Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2004 iweze kufanya kazi kwa asilimia 100.

Amesema kutokuwepo kwa usimamizi wa kutosha kumetoa mianya mingi ya ‘kuweka cha juu’ (over invoicing), utoaji rushwa na uagizaji wa bidhaa feki au duni kupitia manunuzi yanayofanywa na wanataaluma wa fani hali inayoyasababisha upotevu mkubwa wa fedha za umma.

Ametoa kauli hiyo  mjini Arusha leo mchana (Jumatano, Desemba 14, 2011) wakati  akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Pili wa wataalamu wa masuala ya ugavi na manunuzi katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Arusha (AICC).

“Usimamizi ni suala muhimu kama tunataka sheria ya manunuzi ifanye kazi kwa asilimia 100, na wenye dhamana hii ni viongozi wanaosimamia idara na taasisi mbalimbali lakini zaidi ni wale wanaosimamia masuala ya ugavi,” alisema.

Alisema hivi karibuni amewaandikia barua Wakuu wote wa Mikoa ili wawasimamie Wakurugenzi wa Halmashauri kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wakati atakapofanya ukaguzi wake.

“Kwa kawaida CAG huwa anatoa ratiba kuonyesha ni linzi atakagua wizara, taasisi za seikali na mikoa… pia anatoa vigezo vyake kwamaba anataka acute nini kimeandaliwa kwa ajili ya ukaguzi.”

“Nimewaandikia wakuu wa mikoa yote kuwataka wasimamie hilo zoezi na ikibainika katika ripoti ya CAG kwamba kuna Mkurugenzi amepata ripoti chafu kwa sababu hakutelekeza ni lazima tutamshughulikia…”

Alisema Wakurugenzi wanaofanya uzembe na kusababisha ripoti chafu wanasababisha halsmashauri zao zikose fedha za maendeleo. “Hatuwezi kuona mtu mmoja au wawili wanasababisha wananchi wote wakose maendeleo kwa sababu ya matatizo ya mtu mmoja au wawili,” alisisitiza.

Alisema wale wote watakaobainika kuzembea kwanza watavuliwa madaraka yao ya ukurugenzi halafu kama watabainika kuhusika na wizi au upotevu wa fedha za umma itabidi wafikishwe mahakamani.

Mapema katika hotuba yake Waziri Mkuu alisema kwamba asilimia 80 ya bajeti ya maendeleo inatumika katika manunuzi ya Serikali kupitia ununuzi wa bidhaa na huduma pamoja na kupata huduma za ushauri wa kitaalamu (advisory services or consultancies).

Alisema katika ukaguzi ulifanywa kwenye taasisi 174 zinazofanya manunuzi, ni asilimia 68 tu ya taasisi hizo ambazo zilifuata kanuni za manunuzi. Kwa mujibu wa taarifa ya ukaguzi huo, taasisi 39 zilipata asilimia 80, taasisi 115 zilipata alama ya wastani wa asilimia kati ya 50 na 80 wakati taasisi 20 zilipata asilimia chini ya 50.

Aliyataja maeneo sugu kuwa ni Procurement Planning, Establishment of Procurement Monitoring Unit (PMU), Quality Assurance, Contract Management as well as Publication of Awards. (NAOMBA MSAADA WA KUTAFSIRI SBB NATAKA KUANDIKA VERSION YA KIINGEREZA)

Katika ripoti hiyo, jumla ya miradi ya ujenzi 136 ilifanyiwa ukaguzi wa thamani ya fedha kulingana na bidhaa zilizonunuliwa (value for money audits) ambapo miradi 61 ndiyo ilifuata kanuni na taratibu.

“Kati ya miradi 81 ya barabara, miradi 33 ya majengo miradi 13 ya umwagiliaji na miradi saba ya madaraja, ni miradi 61 tu sawa na asilimia 44.9 ndiyo ilitekelezwa kwa mujibu wa sheria. Miradi 51 (43.4%) ilikuwa ni ya kiwango cha wastani na miradi 16 (11.8%) ilitekelezwa vibaya.

Katika ukaguzi huo, Waziri Mkuu alisema jumla ya sh. milioni 238.8 zililipwa kwa miradi hewa katika wilaya za Bahi, Geita, Magu, Mvomero na Sengerema. Alitumia fursa hiyo kuwataka maafisa ugavi na manunuzi wanaoshiriki mkutano huo wa siku tatu kuhakikisha kuwa wanafikia lengo la asilimi 80 lililowekwa na Serikali la kufuata kanuni na taratibu za manunuzi ifikapo mwaka 2013/2014.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: