Mke wa mgonjwa huyo Amina Ramadhan alisema kuwa mme wake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria kwa kipindi cha mwezi mmoja sasa kabla ya jana mgonjwa huyo kuomba kuletwa mjini Iringa kwa mhubiri huyo maarufu mkoani Iringa Boaz Sollo wa kituo cha maombezi cha overcomers.
Hata hivyo alisema kuwa akiwa katika foleni ya kuingia ndani ya ukumbi ghafla mgonjwa huyo aliomba kupelekwa chooni na kabla ya kuingia chooni alikata kauli na hivyo kulazimika kuupeleka mwili wake mochwari katika hospital ya mkoa ambako kabla ya kuingizwa Mochwari ghafla marehemu aliamuka na kuanza kurusha rusha mikono yake hali iliyopelekea kurudishwa tena mapokezi kwa ajili ya kuchunguzwa zaidi na kumtaja mjane wa marehemu Bi Amina Ramadhan alimtaja marehemu kuwa ni Gerald Tadei Ngusi

Tukio hili limetokea majira ya saa 10 za jioni katika ukumbi huo wa IDYDC mjini Iringa na hadi mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com unatoka hospital hapo majira ya saa 11 .20 jioni madaktari walikwisha mpima na kuthibitisha kifo cha mgonjwa huyo.
Picha na habari kwa hisani ya Francis Godwin Blog.

Toa Maoni Yako:
0 comments: