Afrikats ni mradi unaoendeshwa na Tanzania House of Talents kwa ushirikiano na Ubalozi wa Denmark nchini Tanzania. Lengo kuu la mradi huu ni kuhamasisha vijana kutumia sanaa kama njia ya kujiletea kipato na maendeleo yao, pia kama njia ya kukuza na kutunza utamaduni wetu. Mradi huu unawahusisha vijana wenye vipaji vya uimbaji, kucheza na kuingiza kutoka THT, ambao wamepatiwa mafunzo juu ya uigizaji mahairi, kuimba na kucheza. Vijana hawa watazunguka nchi nzima kuwahamasisha vijana wenzao kupitia igizo ambalo limebeba tamaduni mchanganyiko.

Afrikats ilizinduliwa Morogoro ambapo vijana walifanya matamasha saba katika wilaya mbili za Morogoro Mjini na Mvomero kuanzia 21 May hadi 28 May.
Baada ya hapo programu hii ilihamia mkoani Tanga katika wilaya za Pangani, Muheza, na Tanga mjini.

Ujumbe ukiwa kuhamasisha njia bora ya kufanya sanaa kwa kuelimisha na kujipatia kipato. Pamoja pia walishirikiana na Ngoma Afrika katika tamasha la PAUKWA katika uwanja wa Jamuhuri.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: