Serikali imewazawadia wanafunzi bora 20 waliofanya vizuri kwenye mtihani wa kidato cha Sita mwaka huu zikiwemo komputa ndogo, shilingi laki moja na nusu na cheti cha ubora kila mmoja ili kuthamini kazi kubwa waliyoifanya kwa ushirikiano wa walimu na wazazi wao.

Akikabidhi zawadi hizo Bungeni mjini Dodoma mara baada ya kipindi cha maswali na majibu, Waziri Mkuu mheshimiwa Mizengo Pinda alisema licha ya wanafunzi hao, wazazi na walimu waliowafundisha nao watazawadiwa ili kuongeza ari ya kujifunza na kufundisha mashuleni.

Mbali na hatua hiyo serikali pia itatoa meza ya maabara yenye thamani ya shilingi milioni tano na cheti kwa kila shule za kata walikosomea wanafunzi saba kati ya ishirini waliofanya vizuri kwenye mtihani wa kidato cha sita.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: