Serikali imefuta vibali vyote vya kusafirisha mazao ya chakula nje ya nchi ili kuipa nafasi ya kufuatilia mwenendo mzima wa upatikanaji wa chakula nchini.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Profesa Jumanne Maghembe aliliambia Bunge mjini Dodoma kuwa hatua hiyo inakwenda sambamba na kupiga marufuku uuzaji wa mazao yote ya chakula nje ya nchi kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Julai mosi hadi Disemba 31 mwaka huu.
Aidha, Profesa Maghembe alionyesha kusikitishwa kwake na tabia ya wafanyabiashara kununua mazao ya wakulima yakiwa bado shambani akisema kwa kufanya hivyo, wakulima wamapewa bei za chini mno jambo linalowakosesha stahili halisi ya jasho lao.
Kuhusu hali ya chakula Duniani, Waziri Maghembe amesema kuwa taarifa ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa- FAO ya mwezi Mei mwaka huu inaonyesha kuwa katika mwaka 2010/2011, uzalishaji wa nafaka ulitazamiwa kushuka kwa asilimia 1.2
Kushuka huko kwa uzalishaji, Profesa Jumanne Maghembe amesema nchi 30 Duniani zinatazamiwa kukabiliwa na upungufu wa chakula na hivyo kuhitaji chakula cha msaada, nyingi zikiwa Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Toa Maoni Yako:
0 comments: