Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad ameiomba Ghana kupanua wigo wa ushirikiano kati yake na Zanzibar, na kuangalia uwezekano wa kuisaidia katika uimarishaji wa kiwango cha elimu Visiwani humo.

Maalim Seif ametoa wito huo leo visiwani humo wakati alipokutana na na kufanya mazungumzo na Mfalme wa Ashanti, Otumfuo Osei Tutu.

Maalim Seif Shariff Hamad akipokea zawadi kutoka kwa msaidizi wa Mfalme wa Ashanti, Otumfuo Osei Tutu, baada ya kumaliza mazungumzo yao,ofisini kwake Migombani Zanzibar
Amesema ushirikiano baina ya Tanzania na Ghana ni wa muda mrefu wakati ambao Viongozi waasisi wa mataifa hayo Hayati Abeid Karume, Mwalimu Julius Nyerere pamoja na Kwame Nkrumah walipokuwa wakipigania Uhuru wa nchi zao na Afrika kwa jumla.

Amesema katika kuendeleza ushirikiano huo, kuna umuhimu mkubwa kwa Ghana ambayo imefikia maendeleo makubwa, kuisaidia Zanzibar katika kuinua kiwango cha elimu kwa Shule za Sekondari na Msingi zilizopo Visiwani humo.

Vile vile Maalim Seif alitumia fursa hiyo kumuomba Mfalme Tutu kuangalia uwezekano wa kuisaidia Zanzibar katika dhamira zake za kuimarisha huduma bora za afya, akielezea changamoto kadhaa zinazoikabili sekta hiyo, ikiwemo upungufu wa madaktari, vifaa na wataalamu mbali mbali.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: