Mwanamuziki mahiri wa miondoko ya Hip hop ambaye pia ni muigizaji wa Filamu kutoka nchini Marekani ajulikanae kwa jina la  Christopher Brian Bridges aliyezaliwa mnamo  Septemba 11, 1977,ambaye pia anajulikana zaidi kwa jina la kisanii kama Ludacris, anatarajiwa kushuka nchini Tanzania na kuangusha bonge la shoo kwenye tamasha la miaka kumi ya msimu wa dhahabu unaoendelea na serengeti Fiesta 2011.

Akizungumza  na kuthibitisha ujio wa Mwanamuziki huyo mapema leo asubuhi jijini Dar,Mkurugenzi wa Maendeleo na Utafiti wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba amesema kuwa,Mwanamuziki Ludacriss na mwanamuziki mwingine wa kimataifa kutoka nje (atatajwa hapo baadaye),wanatarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha la miaka kumi ya msimu wa dhahabu unaoendelea na serengeti Fiesta 2011 kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar Es Salaam mnamo Julai 30.

Mutahaba amesema kuwa mpaka sasa mambo yanakwenda sawa bin sawia,na kwamba shamra shamra za kufikia kilele cha miaka 10 ya Serengeti Fiesta 2011 itakuwa tofauti na wenye msisimko mkubwa ikilinganishwa na miaka mingine yote iliyowahi kufanyika tamasha hilo, ambalo ni kubwa katika anga ya burudani ndani na nje ya Tanzania ikiwemo Afrika Mashariki kwa ujumla.

Aidha Mutahaba amebainisha pia kwa kutoa shukurani za dhati kwa mikoa ambayo tayari tamasha hilo limekwishafanyika,amewashukuru kwa kujitokeza kwao kwa wingi na kuonyesha ni namna gani tamasha hilo linalowakutanisha watu wa aina mbalimbali na linavyowajengea upendo wa umoja na mambo mengine mbalimbali ikiwemo na kufahamiana.

Mutahaba ameongeza kwa kutoa shukurani nyingi zaidi kwa wakazi wa Mkoa wa Iringa na Mbeya kwa namna walivyojitokeza kwa wingi na kulikubali tamasha hilo ambalo hufanyika mara moja kwa mwaka. "Fiesta ya mwaka huu tumepata sapoti kubwa kutoka kila kona kwa asilimia kubwa,tunamshukuru kamanda wa polisi mkoani Mbeya Kamanda Nyombi,Kamanda wa polisi  Mkoani Iringa ikiwemo na halmashauri zote mbili zilizoshiriki kwa namna moja ama nyingine na  kulifanikisha tamasha la Fiesta 2011 kufanyika katika mikoa hiyo".Alitanabaisha Mutahaba.

"Nisiache pia kuwashukuru wasaniii wote walioshiriki kwenye Mikoa ya Mbeya na Iringa,kwa pamoja nadhani tuko pamoja katika kuijenga Fiesta 2011.Kutokana na ujio wa Wasanii wa Kimataifa kwa sasa timu yetu inaanza kujigawa kwa ajili ya kuweka umakini katika kilele cha tamasha hilo litakalofanyika Julai ,30 katika viwanja vya Lidaz Club.Katika shamrashamra hizo za kutimiza miaka 10 ya Serengeti Fiesta 2011 kutakuwepo na mambo mbalimbali yatakayolinogesha tamasha hilo kubwa hapa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla",alisema

Wiki hii tamasha la Serengeti Fiesta 2011 litakuwa ndani ya wakazi wa mji wa Moshi na Arusha,hivyo wajiandae kujiachia na kupata Majotroozzz ya uhakika kabisa. 
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: