RAMALLAH –Rais wa zamani wa nchi ya Brazil Bwana Luiz Inácio Lula da Silva (pichani) ameteuliwa kuwa mjumbe mahsusi wa nchi hiyo kufanya mazungumzo na Kundi la 77 juu ya kutambuliwa rasmi kwa taifa huru la Palestina kwenye Umoja wa Mataifa.

Brazil, kwa upande wake, tayari imekwisha itambua Palestina kama taifa huru kwa mujibu wa mipaka ya mwaka 1967 ilipofika mwezi Desemba, 2010 hivyo kuongoza njia kwa nchi zote za Amerika ya Kusini nazo kuitambua Palestina.

Nchi zingine ambazo tayari zimeonesha kuiunga mkono Palestina ni: Argentina, Bolivia, Ecuador na Chile na nchi nyingine kadhaa.
Hivi sasa Bwana Lula amejitolea kufanya mazungumzo na viongozi wa nchi zinazoendelea ili ziitambue Palestina haraka iwezekanavyo; ili nayo ipate uanachama wa 194 wa Baraza la Umoja wa Mataifa, mwezi Septemba mwaka huu.

“Lengo hasa la Brazil ni kuleta msukumo wa kisiasa ili Waisraeli na Wapalestina wafikie muafaka kwa njia za kidiplomasia. Lakini kwa hali ilivyo hivi sasa, inaonesha kuwa mgogoro huu utazidi kuendelea hivyo kwa muda mrefu," alisema mshauri wa rais Marco Aurélio García kwa gazeti la O Estado.

Raisi wa Brazil Dilma Rousseff anatarajiwa kutoa hotuba yake kwenye kikao cha mwaka huu cha Baraza la Umoja wa Mataifa na suala la Palestina litakuwa mbele ya ajenda yake.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: