Ubunifu kazini, kama unavyomuona muuza machungwa akiwa ameweka mwamvuli wake kichwani huku akitoa huduma kwa wateja wake.Matunda yanapatikana hata barabarani.Biashara ikifanyika mazingira hatarishi.Jiji la Dar es Salaam kwa sasa linaonekana ni chafu kutokana na kuchafuliwa na wafanyabiashara wadogo wadogo (Machinga) ambao wametanda kila mahali utakuta vibanda na wengine wameweka masoko barabarani hali ambayo inasababisha kuonekana ni uchafu tu, ni vyema wahusika kulifanyia kazi suala hili ambalo limekuwa ni kero kwa mazingira na hata muonekano wa jiji kwa ujumla.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: