Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Grand Malt leo inatangaza rasmi uzinduzi wa promosheni maalum ya ‘Excel With Grand Malt’ kwa vyuo vya Elimu ya juu . Promosheni hii ambayo itakuwa ikifanyika kila mwaka ina lengo la kuwazawadia wanafunzi wa vyuo vya Elimu ya juu waliyotoa mchango kwenye jamii au kufanya vizuri zaidi ya wenzao. Ugunduzi, Michezo, Mazingira na Huduma zaki Jamii, Utamaduni na Burudani.

Kinywaji cha Grand Malt kiliziduliwa rasmi Aprili 28, 2010 na TBL, tangu hapo kinywaji hiki ambacho hakina kilevi, kinaongoza katika bidha zote za aina hiyo (Kimea).

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt, Consolata Adam alisema kuwa washindi wa Tuzo za Excel With Grand Malt watakuwa mabalozi wa kinyweaji hicho kwenye vyuo vyao.

"Leo tunazindua tuzo hizi za Excel With Grand Malt tukiwa na lengo la kuwapatia wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu nafasi ya kupata uzoefu wetu wa kinywaji kisichokuwa na kilevi ambacho kinachangamsha, kuburudisha kikiwa na virutubisho vya aina nyingi Lakitosi pamoja na Vitamini mbalimbali. Kinywaji hiki kinatumiwa wakati wowote ule na kwa kila mtu,” Alisema Consolata

Akiongea katika uzinduzi wa promosheni hiyo, Meneja Miradi Maalum wa TBL, Emma Oriyo alisema kuwa jumla ya vyuo vya elimu ya juu ishirini vitashiriki katika kinyang’anyiro cha tuzo hizo; Alivitaja vyuo hivyo kuwa ni Chuo cha Mzumbe, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Ardhi, Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) , Chuo cha Elimu ya Biashara, Taasisi za Kijamii na Chuo Kikuu Cha Elimu ya Elimu (DUCE).

Kwa mujibu wa Emma, vyuo vingine ni Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo Kikuu cha Elimu Mkwawa na Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa.

Zawadi zitakazotolewa kwa washindi ni, kofia, kalamu, mifuko ya kubebea vitabu, madaftari. Zawadi kubwa itakuwa ni hundi ya pesa kwa ajili ya kununulia vitabu yenye thamani ya Sh. 400,000/-

Emma alisema kuwa mchakato wa kupata washindi utaanza kwa kutaja washindi, kitendo ambacho kitafanyika ndani ya wiki mbili. Baada ya hapo kutakuwa na muda wa wiki moja tena wa kupata watu kumi. Mchakato utaendelea tena kwa wiki mbili tena ili kupata washindi watatu kwa kila kundi.

Mshindi atapatatikana katika tamasha maalum ambalo tarehe yake itatajwa hapo baadaye.

Ili kuchagua mshindi unatakiwa kutuma meseji kupitia simu ya mkononi kwenda namba 0658-517517. Halikadhalika kupitia tovuti ya Grand Malt ambayo ni www.excelwithgranmalt.com. Pia kutakuwa viboksi za kura zitapatikana katika maeneo mbalimbali ya vyuo husika kama vile kwenye maduka, hosteli, kwenye migahawa .
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: