RAMALLAH-- Chama cha Ukombozi wa Palestina (PLO) jana Jumanne kimelilaani vikali Baraza la Congress la Marekani kwa kuutaka Umoja wa Mataifa (UN) kuiondoa ripoti ya ‘Goldstone’ juu ya mauaji yaliyofanywa na utawala wa kibaguzi wa Israeli huko kwenye Ukanda wa Gaza wakati wa mgogoro uliozuka mwaka 2008-2009.
Taarifa iliyotolewa jana na Idara ya Mambo ya Nje ya chama hicho inasema kuwa msimamo huu wa Marekani unadhihirisha kuwa nchi hiyo inaunga mkono utawala wa kibeberu wa Israeli kuendeleza ukandamizaji wake, kuua na pia mpango wake wa kuwanyang’anya ardhi Wapalestina; ukienda kinyume na siasa zake ilizojitangazia za kutowaua raia wasiokuwa na hatia kote duniani kote.
Muswada huo unamtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kufanya marekebisho katika muundo wa Baraza la Haki za Binadamu ili Israeli isishitumiwe kwa kufanya ukatili wa kivita. PLO kinasema kuwa muswada huo unaridhia mauaji ya kinyama yaliyofanywa na Israeli kwa wananchi wa Pslestina kwa kuungwa mkono na utawala huko Marekani.
Kimemtaka raisi wa nchi hiyo Baraka Obama kutoidhinisha vipengele vya muswada huo kwa kuegemea Israeli zaidi, huku ikikiuka sheria zote za kimataifa na kupuuza haki za Wapalestina. Pia kimeitaka jumuia ya kimataifa kuwalinda Wapalestina kwa hali na
Toa Maoni Yako:
0 comments: