New England Umoja inawaletea maonyesho ya mavazi ya kwanza na ya kipekee ya Ki-Tanzania yanayotarajiwa kufanyika Jumamosi hii tarehe 23, 2011 Katika ukumbi wa KNIGHT OF COLUMBUS 484 Lancaster st,MA 01453. Maonyesho hayo kabambe yataanza saa mbili usiku kwa Chakula cha Jioni (Dinner).
"Fashion Show" itaanza Saa 4 Kamili Usiku, na Muziki utafuatia mpaka saa saba usiku. Kiingilio $15 kwa watu wazima na watoto $5.
Maonyesho hayo yamedhaminiwa na Mama Maarufu wa mitindo Tanzania "Aunt" Asia Idarous Hamsini. Ameahidi kutoa burudani ya kupoza Roho!.
Chukuwa tiketi yako mapema kabla hujakosa uhondo!!. Tiketi zipo kwa idadi Maalum. Kwa maelezozaidi kuhusu tiketi gonga www.newenglandumoja.net.
Maandalizi ya Maonyesho hayo yamekamilika yakiwa na washiriki kutoka pande mbalimbali za mikoa ya MA,CT,NH,RI,NY,NJ,DC. wamethibitisha kushiriki Maonyesho hayo ya aina yake.
Pia Katika Maonyesho hayo kutakuwa na mgeni kutoka Bongo ambaye alikuwa kwenye fainali ya Bongo star search "JOSEPH MAIGE" ambae atatoa burudani yake katika jitihada za kuunga mkono N.E.U Foundation.
Burudani ya Muziki pia itatolewa na Ma-DJ wetu Mahiri Rich-Maka na Masudi, na DJ Mualikwa Kutoka DC, si mwingine isipokuwa DJ Luca ambao kwa pamoja watafanya vitu vyao kama kawaida!.
Mnakaribishwa wote kwenye maonyesho hayo ya aina yake.
Toa Maoni Yako:
0 comments: