Kampuni ya Flora Promotions ya jijini Mwanza imeaandaa shindano la kutafuta, kukuza na kuwezesha vipaji vya waimbaji wa muziki wa Injili liitwalo ZABURI GOSPEL SEARCH 2009, ili kueneza neno la mungu kupitia nyimbo.Mkurugenzi wa kampuni ya Flora Promotions ambaye ndiye mratibu wa shindano hilo Bi. Flora Lauwo amefafanua hivi karibuni jijini Mwanza kuwa

“Suala la zawadi liko wazi kabisa, ni kwamba mshindi wa kwanza atajinyakulia gari aina ya Toyota Vistar yenye thamani ya milioni nane, mshindi wa pili ataibuka na seti ya vyombo vya muziki vyenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu kutoka kampuni ya Samila Mobile Sound, mshindi wa tatu atajinyakulia kitita cha shilingi laki mbili, lakini pia mshindi wa kwanza mpaka tano watarekodiwa albamu moja moja na studio za Habari Maalum” amesema Flora.

Flora ameongeza kuwa kwa mara ya kwanza mwaka 2009, kipindi cha ZABURI GOSPEL SEARCH kimeanzia kanda ya Ziwa kwa kutafuta washiriki kila mkoa na kufanikiwa kuibuka na waimbaji watano ambapo jumla wamekuwa 20, anasema na kuongeza kuwa washiriki hao tayari wameingia kambini kujinoa tayari kwa michuano ambayo tayari imekwishaanza anza kurushwa hewani kupitia Star Tv na wananchi kuwapigia kura wakisaidiana na majaji kutafuta mwimbaji bora.

“ZABURI GOSPEL SEARCH 2009 itakuwa na matamasha makubwa matatu moja litakuwa ni robo fainali litakalofanyika mkoani Shinyanga tar 25/12/2009 na nusu fainali itakuwa Musoma mkoani Mara tar. 27.12.2009, na fainali yenyewe itafanyikia jijini Mwanza Januari 1, 2010 siku ya mwaka mpya.

Bi. Flora amemaliza kwa kusema kuwa lengo lao ni kukuza na kuwezesha waimbaji wa muziki wa injili na kuwatangaza Kitaifa na Kimataifa ili waweze kijipatia kipato na kufaidika kwa namna moja ama nyingine kama wasanii wengingine.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: