01:- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia na kupata maelezo kutoka kwa Meja Ali Kitundu, kuhusu elimu ya awali kwa wanafunzi wanaojifunza elimu ya afya kabla ya ajila., wakati alipofika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kufungua Kongamano la Mradi wa Maisha kuhusu Afya ya Mama na Mtoto. Kutoka kulia ni Dkt. Grace Qoro, Waratibu wa mradi huo, Jasmine Chechewa na Shallah Ukende. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo jinsi ya kumhudumia mama mjamzito kutoka kwa Mratibu Msaidizi wa Afya Mzazi na Mtoto wa Wilaya ya Ilala, Edith Mboga, wakati alipofika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kufungua Kongamano la Mradi wa Maisha kuhusu Afya ya Mama na Mtoto. Kulia ni Mshauri wa Ukunga Mradi wa Maisha, Scholastica Chibehe. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia, wakati alipofika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kufungua Kongamano la Mradi wa Maisha kuhusu Afya ya Mama na Mtoto. Picha na OMR
 05:- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti mwakilishi wa Mradi wa Maisha kutoka Mkoa wa Dar es Salaam, Theresa Mmbando, wakati wa ufunguzi rasmi wa Kongamano la Mradi wa Maisha kuhusu Afya ya Mama na Mtoto, jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti mwakilishi wa Mradi wa Maisha kutoka Mkoa wa Morogoro, ambaye ni Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro, Eliya Ntandu, wakati wa ufunguzi rasmi wa Kongamano la Mradi wa Maisha kuhusu Afya ya Mama na Mtoto, jijini Dar es Salaam leo. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti mwakilishi wa Mradi wa Maisha Rasi wa Mkoa wa Singida, Liana Hassan, wakati wa ufunguzi rasmi wa Kongamano la Mradi wa Maisha kuhusu Afya ya Mama na Mtoto, jijini Dar es Salaam leo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waratibu wa Kongamano hilo baada ya ufunguzi rasmi leo jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
Sehemu ya njia ya reli katika eneo la Ming’ongo ikiwa inaning’inia baada ya tuta kusombwa na maji kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Kipalo Amani Kisamfu pamoja na wakurugenzi kutoka Wizara ya Uchukuzi wametembelea eneo hilo leo mchana kuona athari kubwa iliyotokea kwenye njia ya reli. Aidha, katika njia hiyo kilomita kumi na nane za njia ya reli zimeaharibiwa na mvua hizo zinazoendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania.
Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Reli, Wizara ya Uchukuzi, Bw. Festo Mwanjika (wa pili kutoka kulia) akiangalia uharibifu mkubwa uliotokea kwenye njia ya reli katika eneo la Ming’ong’o kilomita 4 kutoka Stesheni ya Ruvu, alipotembelea eneo hilo kujionea moja kati ya sehemu kumi na nane zilizoharibiwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Uchukuzi)

Kiongozi wa Lazima Ukae GYM Gulamu Kassim kushoto akipambana na bondia Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe' wakati wa mazoezi yake yanayoendelea katika kambi hiyo iliyopi Kinondoni Dar es salaam Miyeyusho anajiandaa na mpambano wake na  Bondia SukkasemKietyongyuth  kutoka Thailand April 19 na Mohamed Matumla Mei 10 mipambano yote itafanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba.
Kiongozi wa Lazima Ukae GYM Gulamu Kassim kushoto akimwelekeza bondia Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe' jinsi ya kutupa makonde wakati wa mazoezi yake yanayoendelea katika kambi hiyo iliyopi Kinondoni Dar es salaam Miyeyusho anajiandaa na mpambano wake na  Bondia SukkasemKietyongyuth  kutoka Thailand April 19 na Mohamed Matumla Mei 10 mipambano yote itafanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba.
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya kulipia mafuta kwa Mpesa kwenye vituo vya mafuta vya Total nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara wa Total Romee de Villeneuve. Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dra es salaam.
 Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania,Salum Mwalim akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi ya kulipia mafuta kwa Mpesa kwenye vituo vya mafuta vya Total muda mfupi baada ya kuzinduliwa rasmi kwa huduma hiyo kwenye kituo cha Total cha Morocco jijini Dra es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara wa Total Romee de Villeneuve. Huduma hiyo itakuwa ikipatikana kwenye vituo vyote vya Total hapa nchini.
 Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim (wa pili kushoto) akimsadia dereva Taxi Said Juma kulipia mafuta kwa njia ya M-pesa katika kituo cha Mafuta cha Totola Morocco jijini Dar es salaam akiwa ndie mteja wa kwanza kutumia huduma hiyo muda mfupi baada ya kuzinduliwa kituoni hapo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara wa Total Romee de Villeneuve na kulia ni mhudumu wa kituo hicho Malaki Peter. Huduma hiyo itakuwa ikipatikana kwenye vituo vyote vya Total nchini.
 Wafanyakazi wa Vodacom wa idara ya mauzo wakibandika stika kwenye kituo cha mafuta cha Total Morocco jijini Dar es salaam zinazoonesha nambari ya biashara ya kulipia huduma ya mafuta kwa njia ya Mpesa kituoni hapo. Huduma hiyo imezinduliwa kituoni hapo na kwamba itapatikana kwenye vituo vyote vya Total nchi nzima ikiwa ni mwendelezo wa Vodacom kuwawezesaha watanzania kupata huduma kwa urahisi, uhakika na usalama kupitia huduma ya M-pesa.
Mfanyakazi wa kituo cha mafuta cha Total Morocco jijini Dar es salaam akitoa huduma ya mafuta kwa wateja. Total na Vodacom imezindua ubia wa kibiashara unaowawezesha wateja kulipia huduma ya mafuta kwa M-pesa kwenye vituo vyote vya Total nchi nzima. Huduma hiyo inalenga kutoa unafuu na urahisi wa malipo kwa wateja.
Na Mwandishi Wetu, Lindi.

Tigo leo imefungua duka jipya la huduma kwa wateja mjini Lindiambayo itarahisisha upatikanaji wa huduma zake kwa wateja wa mjini hapo ambao awali walikuwa hawana namna ya kupata huduma za moja kwa moja kutoka kwenye kampuni hiyo ya simu.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi mjini, Kelvin Makonda, ambaye ameipongeza Tigo kwa hatua yake ya kuzidi kusogeza karibu huduma zake kwa watu wa Lindi.

“Pamoja na utatuzi wa kero za mawasiliano naamini ya kwamba duka hili jipya litakuwa kama kituo cha kutoa huduma mbali mbali ambazo wateja wenu wa Lindi watakuwa wanahitaji kutoka kwenu kila siku,” alisema Makonda.

Makonda alisema kwambahuduma mbalimbali za mawasiliano zitolewazo na kampuni ya simu ya Tigo kama vile kupiga simu, kutuma SMS, mtandao wa Intaneti pamoja na huduma ya kutuma na kupokea fedha, zimekuwa kichocheo kikubwa katika kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini. “Aidha huduma hizi zimeleta mageuzi chanya katika ufanyaji biashara na kuinua hali ya maisha ya maelfu ya wakazi wa Lindi na mamilioni ya watanzania kwa ujumla,” alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tigo wa kanda ya Pwani Bw. Brian Kalokola,amesema tawi hilo ambalo linalopatikana Lindi mjini mtaa wa Makongoro karibia na stendi kuulinatarajia kuwahudumia wateja wapatao 150 kwa siku kwa kuwapa huduma mbali mbali za Tigo zikiwemo huduma ya kuunganishiwa intaneti, usajili wa laini za simu, Tigo Pesa na huduma maalum za simu za kisasa (“Smartphones”).

“Duka hili lina manufaa makubwa kwa wateja kwa sababu limeleta huduma zetu karibu zaidi kwao. Pialinapatikana sehemu nzuri kibiashara kiasi kwamba litavutia hata wateja kutokawilaya zingine na maeneo jirani kamaNachingwea, Liwale, Kilwa, Ruangwa na Lindi vijijini,”alisema Kalokola.

Duka hili linatoa huduma nyingine maalum zikiwemouuzaji wa bidhaa mbali mbali kama simu za kisasa ambapo mteja anaruhusiwa kuzijaribisha kabla yakununua. “Hii inamuwezesha mteja kufanya uamuzi sahihi katika kuchagua na kununua bidhaa inayokidhi mahitaji yake.”

Tawi la Lindilinafikisha jumla ya maduka yanayoendeshwa na kampuni ya Tigo nchini kufikia 41. Kwa mujibu wa Kalokola, kampuni hiyo ina mipango yakufungua maduka mengine mengi zaidi katika sehemu mbali mbali nchini.
---
Wafanyakazi wa duka jipya la Tigo la Lindi Mjini katika nyuso za furaha na Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi Mjini Bw. Kelvin Makonda (aliyebeba mfuko wa Tigo) wakati wa uzinduzi wa duka hilo jipya iliyofanyika juzi.
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi Mjini Bw. Kelvin Makonda (kushoto) akimsikiliza kwa makini Meneja wa duka jipya la Tigo lilipo Lindi Mjini Bw. Ahadi Mtweve (katikati) kuhusu huduma ya mauzo ya simu za kisasa pale alipofika kuzindua duka hilo juzi. Duka hilo linalopatikana mtaa wa Makongoro nyuma ya stendi kuu ni duka la 41 la Tigo nchi nzima.
 Meneja wa duka jipya la Tigo lililopo Lindi Mjini Bw. Ahadi Mtweve (katikati) akimuelezea Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi Mjini Bw. Kelvin Makonda kuhusu huduma ya Tigo Pesa inayopatikana kwenye duka hilo mpya liliozinduliwa juzi na Mkurugenzi huyo. Kushoto ni mtoa huduma wa Tigo Pesa katika duka hilo Bi. Nasra Mbise. Duka hilo linalopatikana mtaa wa Makongoro nyuma ya stendi kuu ni duka la 41 la Tigo nchi nzima.
Afisa wa Mahusiano kwa Wateja wa Tigo Bi. Pilila Kavishe (kushoto) na Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi Mjini Bw. Kelvin Makonda (wapili kulia) katika picha ya pamoja na wateja wa Tigo waliozawadiwa kadi za vipaumbele kutoka kampuni hiyo ya simu. Kazi hizo zinampa uwezo mteja wa Tigo kupatiwa huduma za kipekee kama kutokukaa katika foleni anapofika katika duka la Tigo pamoja na kuondelewa kwa gharama mbali mbali anapohudumiwa katika maduka hayo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Kongamano linalohusu Mkakati wa Kimataifa wa Kuboresha Miundombinu katika Ukanda wa Kati (Central Transport Corridor) katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam leo April 15, 2014

Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kongamano linalohusu Mkakati wa Kimataifa wa Kuboresha Miundombinu katika Ukanda wa Kati (Central Transport Corridor) baada ya kulifungua katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam leo April 15, 2014

PICHA NA IKULU.
1
 Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama katikati akiwa katika picha ya pamoja na baba yake mzazi Mzee Mwita na mmoja wa waratibu wa tamasha la pasaka Bw. wakati walipofika katika hospitali ya muhimbili ili kumjulia hali kutokana na majeraha na maumivu ya ajali aliyoipata wiki iliyopita wakati akielekea mkoani Dodoma kwa shughuli zake, watu wengi wamemtembelea hospitalini hapo leo akiwemo Askafu Bruno Mwakibolwa wakanisa la EAGT, Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba na watoto wa kituo cha watoto yatima cha Mwandaliwa, Mbweni jijini Dar es salaam.3Alex Msama akitoka nje ya chumba chake alimolazwa ili kusalimiana na baadhi ya wageni waliomtembelea hospitalini hapo. 6Askofu Bruno Mwakibolwa wakanisa la EAGT akimsalimia Alex Msama wakati aliomtembelea hospitalini hapo kumjulia hali. 7Askafu Bruno Mwakibolwa wakanisa la EAGT akisoma neno takatifu la kumtia faraja Bw. Alex Msama ili aendelee na kazi ya mungu wakati aliomtembelea hospitalini hapo. 9Watoto yatima cha Mwandaliwa, Mbweni jijini Dar es Salaam wakimuombea dua Bw. Alex Msama wakati walipomtembelea katika hospitali ya Muhimbili na kumjulia hali leo 10Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Simon Mwakifwamba akimjulia hali Bw. Alex Msama wakati alipomtembelea katika hospitali ya Muhimbili leo.
 Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza la Marehemu Muhidin Maalim Gurumo wakielekea msikitini kwa ajili ya sala wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo Aprili 15, 2014 kijijini Kwao Masaki.
 Waombolezaji wakisaidiana kupeleka jeneza msikitini.
 Waumini wa dini ya Kiislam wakiswalia Jeneza lilibeba Mwili wa Merehemu Muhidini Maalim Gurumo kabla ya mazishi yake Kijijini kwao Masaki Wilaya ya Kisarawe leo Aprili 15, 2014.
Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania linaloundwa na (Chamudata, Tafoma, Injili, Kizazi Kipya, Asili, Disco), Addo November (mwenye shati ya mikono mirefu) akiongoza waombolezaji kubeba mwili wa marehemu Muhidin Maalim Gurumo wakati wa mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwao, Masaki Kisarawe.
Waombolezaji wakiwa wamefika makabirini.
Taratibu za maziko zikiendelea....
Waombolezaji wakiendelea na zoezi la kufukia udongo kaburi la Marehemu Muhidin Maalim Gurumo.
Mmoja ya wanafamilia akitoka ndani ya kaburi.
Mtoto wa Marehemu Gurumo, Abdallah Muhidin Maalim akisaidiwa kutoka eneo la makabirini mara baada ya kukamilisha zoezi la maziko.
Mbunge wa Bagamoyo, Ridhiwan Kikwete (kulia) akiongea na waombolezaji mara baada ya maziko.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Prof. Jay nae alikuwepo katika maziko hayo.
Waombolezaji wakipiga swala ya mwisho mara baada ya kukamilisha zoezi la maziko.
Ndugu wa Marehemu Gurumo wakomba dua kwenye Kabuli la marehemu Gurumo.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa marehemu Muhidin Maalim Gurumo (mwenye shuka nyeupe) na wanafamilia alipokwenda kuhani msimba huo Ubungo Makuburi jioni ya leo April 15, 2014, siku ambayo marehemu alizikwa kijijini kwao Masaki, Kisarawe, Mkoa wa Pwani.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete pole Bw. Abdallah Muhidin Gurumo, mtoto wa marehemu Muhidin Maalim Gurumo na wanafamilia alipokwenda kuhani msimba huo Ubungo Makuburi jioni ya leo April 15, 2014,
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bw. Omar Muhidin Maalim Gurumo alipokwenda kuhani msimba huo Ubungo Makuburi jioni ya leo April 15, 2014,
 Sehemu ya waombolezaji
 Mmoja wa wana familia Bw. Salim Zagar akitoa taarifa fupi ya msiba pamoja na mazishi kwa Mhe Rais
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Muziki wa dansi Bwana Brighton akimshukuru Rais Kikwete kwa kwenda kutoa pole ya msiba huo.