Na Mwandishi Wetu.
Dodoma, Machi 30, 2026 — Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Jamii, Alex Sospeter Mkama, amekabidhiwa rasmi ofisi ya kuongoza kamisheni hiyo katika hafla iliyofanyika leo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dodoma.
Hafla hiyo ya makabidhiano imeongozwa na aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Ulrich Matei, ambaye alimkabidhi majukumu hayo kwa utaratibu rasmi, akimtakia mafanikio mema katika uongozi wake mpya.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa ofisi, CP Mkama alieleza dhamira yake ya kuendeleza juhudi za kuimarisha ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na wananchi, akisisitiza umuhimu wa jamii kushiriki kikamilifu katika kudumisha amani na usalama nchini.
Kwa upande wake, DCP Matei alisema kuwa ana imani uongozi mpya utaongeza kasi ya utekelezaji wa majukumu ya Kamisheni ya Polisi Jamii, hasa katika kujenga uhusiano chanya na wananchi na kushughulikia changamoto za kiusalama kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Rais wa Kenya, William Ruto, ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo la Ol Kalou, David Njuguna Kiaraho, akieleza kusikitishwa kwake na msiba huo alioutaja kuwa pigo kubwa kwa taifa.
Kupitia ujumbe wake, Rais Ruto amesema mawazo na maombi yake yako pamoja na familia ya marehemu, marafiki pamoja na wananchi wa Ol Kalou katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
Akimzungumzia marehemu Kiaraho, Rais Ruto alimtaja kuwa kiongozi mnyenyekevu, thabiti na mwenye maono, aliyekuwa nguzo muhimu kwa jamii yake kutokana na kujitolea kwake kuwatumikia wananchi wake kwa dhati.
Aliongeza kuwa marehemu atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya elimu pamoja na utumishi wake uliotukuka ndani ya Bunge la Taifa, ambako alisimamia maslahi ya wananchi wake kwa uadilifu.
Rais Ruto pia alibainisha kuwa maisha ya marehemu ni funzo kwa viongozi wa kizazi cha sasa, akiwahimiza kuweka mbele huduma kwa wananchi badala ya siasa zisizo na tija, huku akisisitiza umuhimu wa kuendeleza kaulimbiu yake ya “Kazi Kwanza, Siasa Baadaye.”
Amehitimisha kwa kutoa pole na kumuombea marehemu apumzike kwa amani, huku taifa la Kenya likiendelea kuomboleza kiongozi huyo aliyegusa maisha ya wengi.


Batuli Hemedi Mtendaji wa Kijiji cha Ngukumo wilayani Nzega akipanda moja ya miti iliyotolewa na kampuni ya Tumbaku Alliance One kwa ajili kuchangia zoezi upandaji miti milioni 1.5 wilayani humo sambamba na agizo la serikali.
Na Mwandishi Wetu -Narok, Kenya.
Rais wa Kenya, William Ruto, amempongeza mwanasiasa David Keter maarufu kama Dollarline kwa kushinda katika kura za mchujo za chama cha United Democratic Alliance (UDA) katika Jimbo la Emurua Dikirr Constituency.
Kupitia ujumbe wake, Rais Ruto alimpa pongezi Keter kufuatia ushindi huo muhimu uliompa tiketi ya kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mdogo ujao wa jimbo hilo.
Aidha, Rais Ruto alimpongeza pia mpinzani wake Bernard Ng'eno maarufu kama Buluu kwa kuendesha kampeni imara, akieleza kuwa ushindani huo umeimarisha misingi ya demokrasia ndani ya chama hicho kuanzia ngazi za chini.
“Tunapongeza ushindani wa haki na wa kidemokrasia uliofanyika, ambao unaimarisha chama chetu na kuonesha mshikamano wa wanachama,” ilieleza sehemu ya ujumbe wa Rais Ruto.
Rais huyo alisisitiza kuwa baada ya mchakato wa mchujo kukamilika, ni muhimu kwa wanachama wote wa UDA kuungana na kumuunga mkono mgombea aliyepitishwa ili kuhakikisha ushindi katika uchaguzi mdogo.
“Tunakwenda mbele kama timu moja imara, tukiwa tumeungana nyuma ya mgombea wetu na ajenda ya chama,” aliongeza.
Ushindi wa Keter unatarajiwa kuongeza ushindani mkali katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, huku chama cha UDA kikilenga kuimarisha nafasi yake kisiasa katika Kaunti ya Narok na maeneo ya jirani.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa George Masaju akisaini kitabu cha maombolezo katika ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge,Uratibu na Wenye Ulemavu) Marehemu Mhe. William Lukuvi katika Viwanja vya Karimjee leo tarehe 28 Machi, 2026 Jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha maombolezo katika ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge,Uratibu na Wenye Ulemavu) Marehemu Mhe. William Lukuvi katika Viwanja vya Karimjee leo tarehe 28 Machi, 2026 Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda akisaini kitabu cha maombolezo katika ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge,Uratibu na Wenye Ulemavu) Marehemu Mhe. William Lukuvi katika Viwanja vya Karimjee leo tarehe 28 Machi, 2026 Jijini Dar es Salaam.Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Msanii wa muziki wa hip hop nchini, Wakazi (Webiro Wasira), ameanza rasmi mchakato wa kisheria kupinga hukumu iliyotolewa dhidi yake na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliyomkuta na hatia ya kusambaza taarifa za uongo dhidi ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Baba Levo (Clayton Chipando).
Katika hukumu hiyo, mahakama ilimuamuru Wakazi kulipa fidia ya shilingi milioni 100 pamoja na kumuomba radhi Baba Levo na kukanusha taarifa alizodaiwa kusambaza kupitia mitandao ya kijamii, blogu na YouTube.
Hata hivyo, kupitia taarifa yake kwa umma, Wakazi amesema ameridhia kupeleka shauri hilo mahakamani kupinga uamuzi huo, akidai kuwa hukumu ilitolewa upande mmoja (ex parte) bila yeye kushirikishwa ipasavyo katika mchakato wa usikilizwaji wa kesi.
Ameeleza kuwa tayari amemkabidhi jukumu hilo wakili wake, Peter Kibatala, ambaye ameanza mchakato wa dharura wa kuwasilisha maombi ya kutengua hukumu hiyo ili apewe nafasi ya kusikilizwa.
“Masuala haya yako mikononi mwa wakili wangu, na tayari hatua za kisheria zimeanza kuchukuliwa chini ya utaratibu wa dharura,” imeeleza sehemu ya taarifa ya Wakazi.
Chanzo cha Mgogoro
Mgogoro kati ya wawili hao ulianza baada ya Baba Levo kupoteza begi lenye simu alipokuwa safarini nchini Uturuki. Kufuatia tukio hilo, Wakazi alidai kupitia mitandao ya kijamii kuwa Baba Levo alihusika na wizi wa simu za watu nchini Marekani, madai ambayo baadaye yalikanushwa.
Kwa mujibu wa Baba Levo, uwanja wa ndege wa Istanbul Airport ulimtaarifu kuwa begi lake lilikuwa limepatikana likiwa na vifaa vyote, jambo lililothibitisha kuwa hakukuwa na tukio la wizi kama ilivyodaiwa.
Baada ya hapo, Baba Levo alichukua hatua za kisheria kupinga madai hayo kwa madai ya kuchafuliwa jina, na kesi hiyo kusikilizwa hadi kufikia hukumu iliyotolewa.
Hatua za Sasa
Kwa sasa, Wakazi anapinga hukumu hiyo akisisitiza kuwa hakupatiwa haki ya kusikilizwa kabla ya uamuzi kutolewa. Amesisitiza kuwa hatatoa maoni zaidi hadharani kutokana na unyeti wa suala hilo na kwamba taarifa rasmi zitatolewa na wakili wake kulingana na taratibu za taaluma ya sheria.
Kwa upande mwingine, hukumu ya awali inaendelea kuzua mjadala miongoni mwa wananchi na wadau wa mitandao ya kijamii kuhusu uwajibikaji wa maudhui yanayosambazwa mtandaoni na athari zake kisheria.
Hatua ya Wakazi kupinga hukumu hiyo sasa inaweka wazi kuwa sakata hilo bado halijafungwa rasmi, huku macho ya wengi yakielekezwa kwenye uamuzi wa mahakama kuhusu maombi ya kutengua hukumu hiyo.












.jpeg)



















