Ili uwe mwanaharakati katika jambo fulani, ni lazima usajiliwe katika nchi husika. Kama umefungua shirika la kiraia kitaifa au kimataifa, ni lazima ufanye kazi iliyosajiliwa na si vinginevyo, kama unakuja kumuona rafiki yako, karibu na uende, kwanini unaita waandishi wa habari (Media Press)? Kwanini uzungumzie masuala ya kisiasa katika nchi ambayo wewe sio raia wa nchi hiyo? Tena kwa uchochezi? Lengo ni nini?

Katika sheria ya vyama vya siasa Tanzania ya mwaka 2019 kifungu cha 6C (4) kinakataza mtu ambae sio raia wa Tanzania kushiriki katika chama cha siasa au harakati za kisiasa. Aidha ili uweze kushiriki kazi za uwakili katika nchi yoyote (Participation of advocatism outside territory/Transnational advocacy), unapaswa kuomba kibali kutoka katika nchi husika ili kushiriki kazi za uwakili. Sheria ya uwakili kifungu cha 39-48 kinaeleza wazi uhalali wa kuwa wakili katika mashauri mahakamani. Martha Wangari Karua sio wakili wa kesi husika na hana kibali, Mama Karua sio mtanzania ni raia wa taifa jingine, hana uhalali wa kisheria kuja Tanzania na kushiriki au kuzungumzia masuala ya kisiasa.

Martha Wangari Karua aliwahi kugombea urais wa Kenya 2013 kupitia chama cha National Rainbow Coalition-Kenya (Narc-Kenya) na mgombea mwenza wa Raila Odinga mwaka 2022. Ni mwanasiasa nchini kenya, hakupaswa kuja Tanzania na kuanza shughuli za kisiasa, hakuna mkataba wa kimataifa au wa Afrika ya Mashariki unaoruhusu kuvuka mipaka ya nchi na kufanya siasa pasipo uhalali bila kuwa raia halali.

Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kwakuwa ni mwenye busara, mwanadiplomasia nguli kwa kuzingatia umoja wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki amefanya huruma kumrudisha nchini kwao, alitakiwa Martha Wangari Karua akamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kulipa fine, kufungwa jela au vyote kwa pamoja.

Akajaribu alichokifanya Tanzania huko nchini China, Vietnam na kwingine!!

Na:Mwanasheria Ally Babu (LL. B, LL.M-International Criminal Justice) – 0767126969 

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: