Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki amekutana na kuzungumza na Jumuiya ya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA) waliofanya ziara ya siku kumi na mbili yenye lengo la kutafuta wawekezaji, kujifunza Teknolojia na kuboresha Mahusiano mema ya kibiashara ya Madini ambayo inahusisha zaidi ya Wadau milioni sita Nchini.

Ameeleza kuwa, hii ni kati ya ziara nane zilizofanyika Nchini humo ndani ya miaka sita, mbili zinahusu sekta ya Madini na hii imepewa heshima ya kipekee ya kuagwa na kuongozana na Uwakilishi wa Serikali, ambao uliwakilishwa na Naibu Katibu Mkuu Mhe. Msafiri Mbibo.

Aidha, ametumia nafasi hiyo kuwaaga baada ya kupata Uteuzi wa kituo kipya cha kazi Nchini Uingereza, na kuwahikikishia kuwa Balozi mpya ajaye ni Mtu makini na anaufahamu wa Biashara hivyo ana uhakika yaliyoanzishwa yataendelezwa huku akiwasihi Wafanyabiashara wauze bidhaa kuliko malighafi na kuwatoa wito kwa Mabenki kuwakopesha Wafanyabiashara wa Madini ili kukuza sekta husika

Nae Rais wa FEMATA ameishukuru Serikali na kumuhakikishia Balozi Kairuki kuwa wataendeleza ushirikiano na china, na watakutana na Balozi mpya wa China Mhe. Omar ili kujenga Mahusiano na kuendeleza manufaa ya ziara waliyofanya.

Bina ameeleza kuwa ziara hii imewapa mafunzo, uwezo mkubwa wa kuboresha Sekta ya Madini Tanzania,kufanya biashara kwa urahisi kati ya Nchi mbili , kuboresha Mahusiano kwa kuanzisha Ofisi ndogo ya FEMATA Nchini China na kuingia makubaliano mbalimbali yenye lengo la kuiinua sekta ya madini Nchini.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: