Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) , Dkt. Tausi Kida akizungumza wakati wa ufunguzi wa mjadala wa kisera katika kuadhimisha mwaka mmoja wa Rais Samia ulioandaliwa na ESRF.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Dkt. Hamisi Mkanachi ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akizungumza kwenye mjadala wa kisera katika kuadhimisha mwaka mmoja wa Rais Samia ulioandaliwa na ESRF.
Mtafiti Mshiriki Mwandamizi wa ESRF, Prof. Samuel Wangwe akizungumza kwenye mjadala wa kisera katika kuadhimisha mwaka mmoja wa Rais Samia ulioandaliwa na ESRF.
Mkurugenzi wa masuala ya Kisekta wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Emmanuel Manase akizungumza kwenye mjadala wa kisera katika kuadhimisha mwaka mmoja wa Rais Samia ulioandaliwa na ESRF.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara (Uwekezaji), Bw. Ally S. Gugu akizungumza kwenye mjadala wa kisera katika kuadhimisha mwaka mmoja wa Rais Samia ulioandaliwa na ESRF.
Balozi Modest Mero akizungumza kwenye mjadala wa kisera katika kuadhimisha mwaka mmoja wa Rais Samia ulioandaliwa na ESRF.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) akizungumza kwenye mjadala wa kisera katika kuadhimisha mwaka mmoja wa Rais Samia ulioandaliwa na ESRF.
Baadhi ya wajumbe wa mjadala wa kisera katika kuadhimisha mwaka mmoja wa Rais Samia wakichangia mada.
Washiriki wa mjadala wa kisera katika kuadhimisha mwaka mmoja wa Rais Samia wakiwa wamesimama kwa dakika moja kumkumbuka Rais wa awamu ya tano, hayati Dkt. John Magufuli ambaye ametimiza mwaka mmoja tangu kufariki kwake.
Na Mwandishi Wetu.
ESRF yampongeza Rais Samia kwa mafanikio makubwa ndani ya mwaka wa kwanza
Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imempongeza Rais wa Awamu ya Sita wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ambayo ameifanya katika kipindi cha mwaka mmoja tangu aingie madarakani.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Dkt. Tausi Kida katika mjadala wa kisera ambao umefanyika katika kuadhimisha mwaka mmoja wa Rais Samia ulioandaliwa na ESRF.
Dkt. Kida alisema kwamba kumekuwa na mafanikio makubwa katika maeneo mbalimbali jambo ambalo litaisaidia Tanzania kupiga hatua kubwa katika maendeleo kwa nchi na mwananchi mmoja mmoja.
“Malengo makuu ni kuangalia mafanikio ya kisera ambayo yamepatikana katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Ramia, pia kupata nafasi ya kujadili safari letu ya mafanikio kama mnavyojua mafanikio ya nchi yanahusisha wadau mbalimbali,
“Ukiangalia kwenye kipindi cha mwaka mmoja Rais amefanya mambo makubwa, ukiangalia hata hali ya kiuchumi kila kitu kinaenda vizuri. Kwakweli anastahili pongezi nyingi sana.” alisema Dkt. Kida.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Dkt. Hamisi Mkanachi ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, alielezea namna Rais Samia alivyoleta mabadiliko makubwa ya maendeleo katika wilaya ambayo anaiongoza.
Alisema kumekuwa na miradi mingi ambayo inatekelezwa tangu Rais Samia aingie madarakani, hivyo amewataka wananchi kutumia fursa katika miradi hiyo ili kujitengenezea kipato.
“Mhe. Rais ana utu, anajali haki za watu. Nimekuwa Mkuu wa Wilaya kwa miezi 6 au 7 kwahiyo haya ni yale ambayo mimi nimeyaona. Kwenye utoaji wa huduma hakuna wa kumlinganisha, mfano kwenye bajeti ya barabara za TARURA wilayani kwetu bajeti imepanda kutoka Tsh. 2 bilioni hadi Tsh. 4 bilioni.” alisema Dkt. Mkanachi.
Pia alizungumzia namna uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita unavyofanikisha Mpango wa Maendeleo ya Uchumi (LED) katika sekta ya elimu, miradi ya kimkakati na afya ambayo kwa pamoja itasaidia kukukuza uchumi wa nchi na maendeleo kwa wananchi.
Awali akitoa taarifa kuhusu mafanikio ya Rais Samia, Mtafiti Mshiriki Mwandamizi wa ESRF, Prof. Samuel Wangwe alisema licha ya kwa madarakani kwa muda mfupi lakini mafanikio ni mengi.
“Ukuaji wa uchumi katika sekta mbalimbali za uchumi hususani baada ya janga la ugonjwa wa Korona. Lakini pia ameondoa vikwazo vya kibiashara, uhusiano na wawekezaji umeimarishwa. Hata anapofanya safari zote anakuwa na wafanyabiashara, alisema Prof. Wangwe.
Kwa upande wa Balozi Modest Mero ambaye aliwasilisha mada namna Rais Samia alivyoboresha uhusiano wa kimataifa na diplomasia ya uchumi alisema kuwa kazi kubwa imefanywa na Rais na baada ya kipindi kifupi Watanzania wataona mabadiliko makubwa ambayo yametokana na ziara za Rais alizofanya hivyi karibuni kwenye mataifa makubwa duniani.
Toa Maoni Yako:
0 comments: