Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KAMPUNI ya michezo ya kubashiri ya Parimatch kwa kushirikiana na balozi wao Msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' wametoa msaada wa chakula, vifaa vya kujifunzia kwa makao (vituo vya kulelea watoto yatima) Jijini Dar er salaam.
Tukio hilo limefanyika leo na Kituo cha Huruma Islamic pamoja na Amani Foundation kukabidhiwa vitu hivyo mbele ya waandishi wa habari.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi mtendaji wa Parimatch Tanzania Tumaini Maligana amesema Kmapuni ya Parimatch imejengwa kwa misingi ya kusaidia jamii hususani katika nyanja za elimu, michezo na mazingira.
Amesema, nguzo kuu ni kujali na kukilinda kizazi cha baadae na hivyo Parimatch imeanza kwa kuzingatia idara ya elimu kwa watoto wenye mahitaji muhimu kwa kuwapatia baadhi ya mahitaji hayo.
"Leo tunaanza na vituo viwili vya Mkao ambavyo ni Huruma Islamic na Amani Foundation vyote vikiwa Dar es Salaam na katika mahitaji tutatakayowapatia leo ni pamoja na Chakula na nyenzo za kujifunzia ili kuendana na kasi ya teknolojia" amesema
Aidha, amesema mbali na kuwapatia vitu hivyo lengo ni kuwaandaa vyema na mahitaji ya soko ya ajira kwa kuwapa Luninga, Jenereta pamoja na mifumo kamilifu itakayounda maabara za kompyuta ili viweze kuwaendeleza katika masuala ya elimu na kujifunza.
Balozi wa Parimatch Diamond Platinumz ameweka wazi furaha yake ya kufanya kazi na kampuni hiyo yenye misingi ya kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu hususani Yatima na misingi ya kusaidia jamii katika nchi zote zaidi ya 15.
Diamond amesema, Misingi hiyo ni katika nyanja za elimu, michezo na mazingira, Hivyo leo wanakabidhi msaada huo kwa viongozi wa makao (vituo vya watoto wenye mahitaji muhimu) kama ishara ya program endelevu kusaidia jamii.
Ameeleza "kwa Mkoa wa Dar es salaam kuna vituo vya makao zaidi ya 40 ila tunaanza na vituo viwili kuwapa mahitaji ya chakula ambayo bila hivyo huwezi kusoma, lakini mada kuu ni elimu na Katika elimu sasa tunawatengenezea maabara ya kompyuta yenye kompyuta 10 au zaidi kwa kila kituo na luninga mbili mbili ili hawa nao wasome kitandawazi, wasome kwa fursa sawa kama watoto wengine sio unafundishwa kompyuta kwa kuchorewa ubaoni na mkikwama milango iko wazi karibuni."
Naye Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kituo cha Huruma Islamic Hamisa Mwinyipembe anmewashuruku Kampuni ya Parimatch kwa kuona umuhimu wa kuwasaidia mahitaji muhimu kwa ajili ya vijana wao waliopo katika kituo hicho.
Hamisa amesema, kwa sasa ana watoto 45 ambapo wengine tayari wameshaanza kujitegemea , wengine wakiwa wanasoma vyuo vya elimu ya juu.
Amewaomba makampuni mengine kujitokeza kuwasaidia kwani bado wanahitaji msaada wao ili kuwasaidia watoto hao kwa kupata elimu, chakula na hata malazi kwani kituo hicho hadi sasa hakina nyumba bali kimepanga wakiwaomba wahisani kuwanunulia kiwanja ili waweze kujenga nyumba yao wenyewe.
Balozi wa Parinatch na Msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' akimueleza kitu moja ya watoto waliofika katika hafla ya kukabidhiwa msaada na Kampuni ya Parimatch iliyofanyika leo Jijini Dar es Saalaam.
Balozi wa Parinatch na Msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya kutoka makao (vituo vya kulelea watoto yatima), viongozi wao na Mkurugenzi mtendaji wa Parimatch Tanzania Tumaini Maligana leo wakati wa kukabidhi msaada ya chakula na vifaa vya kujifunzia
Mkurugenzi mtendaji wa Parimatch Tanzania Tumaini Maligana (watatu kulia)akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi msaada ya chakula na vifaa vya kujifunzia kwa makao (vituo vya kulelea watoto yatima), hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Balozi wa Parinatch na Msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' akiwa na Meneja wake Salaam Sk (Kulia) leo Jijini Dar es Salaam.
Msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi msaada ya chakula na vifaa vya kujifunzia kwa makao (vituo vya kulelea watoto yatima) leo Jijini Dar es Salaam, kulia ni Meneja wake Salaam Sk na kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa Parimatch Tanzania Tumaini Maligana leo Jijini Dar es Salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments: